Saturday, December 28

HABARI PICHA: Uzinduzi wa Baraza la Manispaa Chake Chake.

MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, akiwaongoza viongozi mbali mbali wa serikali katika wimbo maalumu wa sisi sote tumegomboka, mara baada ya kuwasili katika hafla ya uzinduzi wa Baraza la Manispaa Chake Chake, hafla iliyofanyika katika viwanja vya kufurahishia watoto Tibirinzi.
WAKUU wa Wilaya nne za Pemba, makatibu Tawala, wakurugenzi wa baraza la Mjini na Halmashauri, wakifuatilia kwa makini hafla ya uzinduzi wa baraza la Manispaa Chake Chake, hafla ya uzinduzi wa Baraza la Manispaa Chake Chake, hafla iliyofanyika katika viwanja vya kufurahishia watoto Tibirinzi.
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, maafisa wadhamini kutoka taasisi mbali mbali za Serikali na wakuu wavikosi vya ulinzi na usalama Pemba, wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Baraza la Manispaa Chake Chake, hafla iliyofanyika katika viwanja vya kufurahishia watoto Tibirinzi.
WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Madungu Wilaya ya Chake Chake, wakiimba wimbo maalumu wa uzinduzi wa baraza la Manispaa Chake Chake, hafla iliofanyika katika kiwanja cha kufurahishia watoto Tibirinzi Wilaya hiyo.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, akitoa salamu za wananchi wa mkoa huo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza la Manispaa Chake Chake, hafla iliyofanyika katika viwanja vya kufurahishia watoto Tibirinzi
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Idara Maalumu za SMZ Massoud Ali Mohamed, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza la Manispaa Chake Chake, hafla iliyofanyika katika viwanja vya kufurahishia watoto Tibirinzi.

MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, akizungumza na wananchi na wafanyakazi wa baraza la Mji wa Chake Chake, kabla ya uzinduzi wa Baraza la Manispaa Chake Chake, hafla iliyofanyika katika viwanja vya kufurahishia watoto Tibirinzi.

 

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)