Saturday, December 28

Wasaidizi wa sheria wakumbushwa juu ya uwepo wa mabadiliko ya sheria.

 

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA

AFISA Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba Ali Salim Matta, amasema sheria ni msingi wa utawala bora katika taifa lolote, kwani moja kati ya nyezo zinazoongoza utawala bora ni uwepo wa sheria katika nchi husika.

Alisema kutokana na hilo ndio maana viongozi wa kuu wa SMT na SMZ, siku hadi siku wamekuwa wakifanya marekebisho na hata kutungwa kabisa kwa sheria mbali mbali kupitia vyombo husika.

Mdhamini huyo aliyaeleza hayo, katika mkutano wakukumbushia kwa wasaidizi wa Sheria na watoa msaada wakisheria upande wa Pemba, uliofanyika nje ya mij wa Chake Chake na kuandalia ya Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar kwa ufadhili wa UNDP.

Aidha alisema hali hiyo inaonesha wazi kuwa nchi inaongozwa na misingi ya utawala bora, na kama kusingekua na sheria nchi isingetawalika, hali ambayo hivi sasa kila mtu anafanya shuhuli zake ipasavyo.

Mdhamini huyo, alisema wasaidizi wa sheria wanakazi kubwa, kwani kazi iliyopo mbele yao ni kuona sheria ambazo viongozi wanazianzisha, zinazotungwa siku hadi siku basi wanajukumu kubwa la kuzifanyia kazi.

Alisema wasaidizi hao wanatakia kuzitafsri kwa usahihi na umakini, ili wananchi waweze kuzielewa na kunufaika, kwani zipo sheria nyingi zinaanzisha na nyengine kufanyiwa marekebisho ili ziwezi kujulikana.

“Hapa nimesikia sheria nyingi zinatajwa ikiwemo, ikiwemo ya sheria ya masuala ya wazee, kanuni za malipo za papo kwa papo ya serikali za mitaa za mwaka 2020, sheria ya ushindani na kumlinda mtumiaji, sheria za kuwawezesha wananchi kiuchuni,”alisema.

Hata hivyo alisema sheria zote hizo zimegusa watu moja kwa moja, maendeleo, amani, usalama wa nchi pia umegusa, hivyo wasaidizi wa sheria wana wajibu wa kuzielewa na kuzifanyia kazi ipasavyo.

Katika hatua nyengine Mdhamini Mata, aliwataka wasaidi hao wa sheria kutambua kua, sheria hizo zinafanya kazi ipasavyo, pamoja na kueleweka kwa jamii, chini ya idara yao ya katiba na msaada wakisheria Zanzibar.

“Sheria hizi ziwe zinafanya kazi ipasavyo bila ya kumuonea mtu yoyote, bila ya kuleta changamoto na kuona haki inatendeka katika ngazi tafauti katika maeneo yao,

Aidha alisema kumekuwa na changamoto mbai mbali katika jamii, ambapo wasaidizi wa sheria wananafasi kubwa ya kupunguza changamoto hizo, ulimwengu umekua na changamoto kubwa ya udhalilishaji kila mmoja anatakiwa kuiangalia kwa umakini ili kupambana na hali hiyo.

“Tunapokua mitaani huko sheria zipo na kama hatutakua makini  zitaendelea kuwepo, vitendo vitaendelea kutokea na wanaohusika watakua hawatiwi hatiani, tukienda kutafsiri sheria basi tutaondosha matatizo hayo,”alisema.

Aliwataka kuwaelimisha jamii juu ya namna nzuri ya kununua ardhi, kwani itapunguza migogoro na kuendelea kudumisha amani na utulivu kwenye jamii.

Aliwahimiza wasaidizi wa sheria kujifunza siku hadi siku juu ya masuala mbali mbali ya sheria, kwani mafunzo hayo sio kama yanatosha bali wanapaswa kuwa na nguvu ya pamoja kuweza kuelimisha na kufikia malengo.

Mapema akitoa salamu Afisa Mdhamini Ofisi ya Rais Katiba sheria Utumishi na utawala bora Pemba Halia Khamis Ali, alisema Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria imekua na kawaida ya kuhakikisha watoa msaada wakisheria wanapatiwa mafunzo elekezi ili kuwajenga kiuwezo zaidi.

Alisema inafanywa hivyo kutokana na mabadiliko yanayotokea ikiwemo ya sheria, ili kujengwa zaidi na kupata uwelewa zaidi juu ya masuala ya sheria na kwenda kusaidia katika jamii.

“Hawa watu wanatusaidia sana na kuhakikisha haki inapatikana katika jamii, wao wanawaongoza wananchi waanze wapi na wafikie wapi, hawa ni watu muhimu katika nchi yetu,”alisema.

Nae Mkurugenzi wa idara ya Katiba na Masaada wakisheria Zanzibar Hanifa Ramadhan Said, alisema uwepo wa mafunzo hayo ni kuwakumbusha juu ya sheria mbali mbali zinazobadilika na watoa msaada wakisheria sio kama wanazifahamu.

Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Skuli taaluma Msemo Mavare, alisema kila mda iliyotajwa hapo inaumuhimu wake katika jamii, kwani ndio wanaookua mstari wambele katika kutoa msaada kwa jamii.

MWISHO