NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.
AFISA Mdhamini Ofisi ya Rais Katiba sheria Utumishi na utawala bora Pemba Halima Khamis Ali, amesema Taifa linafanya kila njia ili kuona jamii inaondokana na changamoto mbali mbali ikiwemo upatikanaji wa haki.
Mdhamini huyo alisema tasnia ya sheria haina kikomo na kuna sheria nyingi zinafanyiwa mabadiliko, hivyo ni wajubu wa wasaidizi wa sheria kujua sheria hizo na kuanza kuzifanyia kazi.
Afisa mdhamini Halima aliayeleza hayo mjini Chake Chake, wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku tatu kwa wasaidizi wa sheria na watoa msaada wakisheria, yaliyoandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wakisheria Zanzibar kwa kushirikiana na skuli ya sheria Zanzibar kwa ufadhili wa UNDP.
“Mabadiliko yote haya kwa sababu mahitaji ya jamii yanazalishwa, mazingira ya jamii yanabadilika na dunia inaseponga mele kulingana na mabadiliko yaliopo,”alisema.
Alisema bahati walionayo wasaidizi wa sheria ya kujazwa kila kitu kinachotokea katika ulimwengu huu, juu ya masuala ya sheria ni bahati ya dhahabu, huku akiwataka kuyachukilia mamafunzo hayo na upepo kwa kwenda kuwatayarisha na kufanya kazi kwa vitendo.
Hata hivyo aliwasihi wasaidizi hao wa kisheria, kwenda kusaidia jamii katika kuhakikisha wanawaokoa dhidi ya udhalilishaji au uonevu wanaofanyiwa kwa kutokuelewa kwao.
Akiwasilisha mada juu ya sheria ya ushindani na kumlinda mtumiaji Zanzibar, Mwanasheria Seif Mohamed alisema biashara ya mtandao Zanzibar bado haziekewa mkazo bado sheria inayozitambua biashraa hizo.
Nae msaidizi wa sheria kutoka Wete Said Rashid, alisema ili kuondosha msongamano wa taasisi nyingi kudai kodi bandarini vizuri kuka na kituo kimaoja tu kitakacho pokea fedha zaote.
“Leo mzingo unaotokana nao Unguja kuupelekea Pemba, gharama zake za ulipaji bandarini unaweza kuona kama unaununua upya, hili tayari baadhi ya wafanyabiashara hao wamehama nakuondosha kuleta bishaa Pemba, halafu mfanya biashara asipandishe bei bidhaa zake,”alisema.
Kwa upande wake Msaidizi wa sheria jimbo la Kiwanja Massoud Abdalla Massoud, alisema wasaidizi wa sheria hao wamefarajika sana kupatiwa mafunzo hayo kwa siku tatu ambayo yamewaongezea ari katika ufanyaji wa kazi zao.
Aidha alimuomba mdhamini huyo kuhakikisha wasaidizi wa sheria wanapatiwa ofisi zao ndani ya ofisi mpya za masheha zitakazojengwa ndani ya wilaya mbali mbali.
MWISHO