NA AMINA AHEMD-PEMBA.
MWENYEKITI wa umoja wa wanawake UWT Taifa Mery Pius Chatanda amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Dr. Hussein Ali Mwinyi ya kujenga miradi mikubwa ya Maendeleo kwa wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba na kueleza Ilani ya CCM anaekeleza kwa kasi kubwa mno ambayo haikuwahi kutokea.
Akizungumza kwa nyakati tofauti Mwenyekiti huyo wa UWT amempongeza Rais Dkt Mwinyi pamoja na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dr. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi na kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo kwa wananchi ndani ya mkoa huo.
Amesema kasi ya ujenzi wa maendeleo katika miradi iliyomo ndani ya mkoa huo itasaidia kuongeza zaidi uhai wa chama na jumuiya zake sambamba na kuendelea kuwatumikia wananchi kwa kuitekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi kwa Asilimia 100.
Kwa upande wake akiwa katika kukagua mradi wa ujenzi wa Skuli ya ghorofa huko Kiwani Makamo Mwenyekiti wa UWT Zainab Khamis Shomari amesema haoni dalili za upinzani kufurukuta kufuatia miradi wenzeshi ya Maendeleo inavyoendelea kujengwa na serikali inayongozwa na Rais Dkt. Samia na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya siasa Mkoa huo amesema katika kujali hali za wananchi wa kisiwa cha Pemba Serikali ya CCM inaendelea kuboresha hali za wananchi kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma bora.
Nao baadhi ya Wakuu wa taasisi za serikali zilizopata kutembelewa na viongozi hao wamesema suala la utatuzi wa kero mbali mbali za wananchi wamekuwa wakizipa kipaumbele kufuatia maelekezo yanayotolewa kwao na Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi na kwa sasa kero nyingi zimeshapatiwa ufumbuzi huku jengine zikiendelea kwa kasi kubwa.
Akielezea utekelezaji wa Ilani ya CCM ktk miundombinu ya Elimu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Leila Moh’d Mussa amesema Rais Dkt Mwinyi tayari ashatekeleza kwa zaidi ya asilimia 150.
Mwenyekiti huyo ametembelea mradi wa nyumba za madaktari, Eneo la maegesho ya makontena na mizigo bandari ya Mkoani, ujenzi wa ZSTC Madungu, Ujenzi wa skuli Michakaini, ukarabati wa uwanja wa Gombani ambapo pia ziara hiyo imetembelea miradi mbali mbali ya maendeleo ndani ya mkoa huo sambamba na kukabidhi kadi kwa wanachama 50 za wananchama wapya wa umoja huo.
Mwisho