NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
HATIMAE Timu ya shehia ya Chamboni imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya MGENI NDONDO CUPO, baada ya kuitandika timu ya Makangale bao 1-0.
Mchezo huo wa fainali uliopigwa katika viwanja vya shamemata Wilaya ya Micheweni, huku ukihudhuriwa na mashabiki wengi wa wakuu wa mikoa, Wilaya, Kamishna wa ZRA na maafisa wadhamini Pemba.
Fainali hiyo iliyovuta hamasa kwa mashabiki wengi na kujizoea umaaruku, kutokana na timu zilizotinga fainali kutokupoteza hata mchezo mmoja ndani ya mashindano hayo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mwaandaaji na mdhamini wa mashindano, Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya, alisema lengo na mashindano hayo ni kupinga udhalilishaji, utoroa wa watoto mashuleni, mimba umri mdogpo, kukataa madawa ya kulevya, ajira za utotoni na kuhamasisha kudai risiti za kieletronik kila mtu anapofanya manunuzi.
Nae mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Leila Burham Ngozi, alisema michezo huhimiza maendeleo, umoja na mshikamano ndio maana viongozi wa nchi wameipa kipaombele kwa kukujengwa na kufanyiwa ukarabati viwanja vya michezo Unguja na Pemba.
“Sote ni Mashahidi uwanja wa Amani hivi sasa unafanyiwa ukatrabati mkubwa, pamoja na uwanja wa Gombani itakapokamilika basi tutakua na viwanja vya kisasa zaidi, lakini sote tunajua kama hizi ni juhudi za viongozi wetu”alisema.
Aliwataka wanamichezo kutumia michezo katika suala zima la kuhamasisha kudai risiti za kieletronik, ili serikali iweze kupata mapato yake.
Mapema Kamishna wa ZRA Zanzibar Yussuph Juma Mwenda, aliahidi msimu ujao wa mashindano hayo, timu zote 28 kuzipatia jezi zitakazokua na ujumbe wa kuhamasisha kudai risiti za kieletroniki, pamoja na ZRA kudhamini mashindano hayo.
Katika fainali hiyo Mshindi wa kwanza shehia ya Chamboni ilipata zawadi ya kikombe, Milioni moja, seti ya jezi na mipira, huku mshindi wa pili akipata laki saba na nusu, jezi na mipira.
Timu yenye nidhamu katika mashindano yao Shehia ya Kinowe, huku mchezaji bora akiibuka Kombo hamad kombo, mchezaji bora chipkizi Suleiman Abdalla kutoka Kipange, nafasi ya Ufungaji bora ikaenda kwa Ali Seif Abdalla kutoka Kifundi, kipa bora akachaguliwa Ali Saleh kutoka Chamboni.
MWISHO