Thursday, January 30

Wadau watoa maoni juu ya rasmi ya sera ya msaada wa kisheria

 

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA

 

WADAU wa Sheria Kisiwani Pemba, wamesema tatizo kubwa lililopo katika Visiwa vya Zanzibar ni kutunga Sheria nyingi, baadae wananchi wanashindwa kutekeleza yale ambayo yanatakiwa.

 

Wakichangia katika Mkutano wa kukusanya maoni juu ya rasimu ya sera ya msaada wa kisheria, ulioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wakisheria Zanzibar na kufanyika mjini Chake Chake.

 

Mmoja ya wadau walichangia rasimu ya sera hiyo, Yussuf Abdalla Ramadhani kutoka jumuia ya KUKHAWA, alisema shida iliyopo ni utekeleza wa Sheria, licha ya Zanzibar kuwa na sheria nyong..

 

Alisema kuwa Sheria, kanuni zimekuwa zikitungwa lakini utekelezaji umekuwa ukisuasua, jambo ambalo linaleta sitofahamu kwa jamii.

 

Nae Massoud Ali Massoud kutoka Ofisi ya Wakfu na Mali amana Pemba, alisema ni vyema kwa wanaotoa msaada wa kisheria kupatiwa motisha, baada ya kuanzishwa kwa mfuko wa watoa msaada wa kisheria.

 

Alisema kuwa watoa msaada wakisheria wamekuwa wakifanya kazi kubwa katika mazingira magumu, hivyo ni vyema pale ambapo mfuko huo utaanzishwa Zanzibar ni vizuri kukawekwa kifungu kwa ajili yao.

 

“Kama ni kujitolea basi hawa watoa msaada wa kisheria wameshajitolea sana, ukiangalia mazingira ya hapa petu kuna changamoto nyingi, endapo huu mfuko kama utafanya kazi ni vyema kuweko na kifungu maalumu kwa ajili ya watoa msaada huo,”alisema.

 

Nae ASP Hassan Khamis Juma kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, alisema ni vizuri katika rasimu hiyo vikashirikishwa vikosi vyote vya Maalum za SMZ, ZAECA na kitengo Cha Madawa ya kulevya katika suala zima la kushughulikia wahalifu.

 

Mapema akifungua mkutano huo Mkurugenzi Idara ya Utawala Bora, pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, Zaina Daud Khalid alisema rasimu hiyo imekuja baada ya kuona kuna changamoto nyingi na mabadiliko ya sayansi na teknologia.

 

Aidalisema mategemeo yao ni kuona wadau wa Sheria Pemba, wanatoa michango mizuri ambayo itaifanya rasimu ya sera ya msaada wakisheri inakuwa yenye kiwango.

 

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya kupitia Rasimu ya sera ya Msaada wakisheria Juma Khamis, alisema mapendekezo yote ambayo yametolewa na washiriki hao, watayachukuwa na kuyafanyia kazi ili waweze kupata rasimu iliyo Bora.

 

Mkutano huo umeandaliwa na idara ya katiba na msaada wakisheria Zanzibar kwa ufadhili wa UNDP.

 

 

                MWISHO.