NA AMINA AHMED-PEMBA.
JUMLA ya wageni (167) kutoka mataifa 14 leo hii wamewasili kisiwani Pemba kwajili ya kutembelea na kujionea vivutio mbali mbali ikiwa ni mara ya nne katika kipindi cha miaka 3 mfululizo kisiwa hicho kupata ugeni wa aina hiyo .
Wageni hao waliopokelewa kwa sherehe mbali mbali ikiwemo ngoma zenye asili ya kisiwa cha Pemba Dufu, pamoja na ngoma aina ya Bosso Ilikuwa ni miongoni mwa mambo yaliyowafurahisha wageni hao kwa kiasi kikubwa jambo ambalo liliwalazimu kuungana na wenyeji wao katika kuzicheza ngoma hizo.
Wakizungumza na habari hizi mara baada ya kuwasili katika bandari ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba baadhi ya wageni hao akiwemo Juliana David,, Silvie Bruno, United states Rodney wareen, Christian Shikardo kutoka Brazil wamesema kuwa mavazi ya utamaduni ,ukarimu mandhari ngoma pamoja na popo ni miongoni mwa vitu vya kipekee vimewavutia katika kisiwa cha Pemba.
Aidha wageni hao wameahidi kutangaza utalii huo waliojionea kisiwani humo katika mataifa yao na kuahidi kurudi katika kisiwa hicho kwajili ya kutembelea vivutio vyengine.
Akizungumza Afisa mdhamini wizara ya Utalii na mambo ya kale Pemba Zuhura Mgeni Othman amesema wizara tayari imeandaa mazingira mazuri kwajili ya wageni hao ambao wamefika kisiwani humo ili watakaporejea nchini mwao kuwa mabalozi wa zuri katika kutangaza utalii wa kisiwa cha Pemba.
Aidha amesema juhudi hizo za kukifungua kisiwa cha Pemba kwa ajili ya shughuli za Utalii na kuongeza kipato kwa taifa zinaendelea kufanywa na Rais wa awamu ya nane Dr Hussein Ali Mwinyi kwa kuimarisha maeneo mbali mbali yenye vivutio vya utalii ndani ya kisiwa hicho.
Hata hivyo mdhamini huyo amewataka watalii wa nje ya nchi pamoja na wa ndani kuendelea kutembelea katika vivutio mbali mbali vinavyopatikana kisiwani humo kujionea vitu vizuri ikiwemo pango za kihistiria Popo wa Pemba na makumbusho mbali mbali.
Watalii hao Kutoka, Brazil, Italy,United King dom, Canada, Germany, United States, France, Hong con , Australia, South Africa, Russian, Swizland, Philipins, Tanzania, ambapo 66 kati yao ni kutoka nchi ya Uphilipino,
58 wakiwa ni wageni na 109 wakiwa ni mabaharia huku Urassa Zakaria Akiwa ni mgeni alieungana na wageni hao Kufanya utalii ndani ya nchi yake ya Tanzania.
Mwisho