Saturday, December 28

UTPC KUHAKIKISHA UMMA UNAELEWA JUU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI.

NA FATMA HAMAD –PEMBA.

Waratibu wa Klabu za Wandishi wa habari Tanzania wametakiwa kuendelea kuratibu na kutoa tarifa za matukio ya ukiukwaji wa uhuru wa kupata na kutoa tarifa na madhila yanayo wapata wandishi wa habar kwenye Mikoa yao.

Wito huo umetolewa na Rais wa Umoja wa Vilabu vya wandishi wa habar Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo wakati akifungua mdahalo wa siku moja kwa njia ya mtandao katika kuadhimisha siku ya kitaifa ya kukomesha uhalifu dhudi ya wandishi wa habari .

Amesema wandishi  wa habari wamekua wakikumbwa na changamoto kadhaa ikiwemo Kushambuliwa, kunyimwa tarifa, hivyo nijukumu lenu waratibu kuripoti pindi ikitokea mwandishi amepatwa na vitendo hivyo ili kuona vinachukuliwa hatua na kuondoka kabisa.

“Waratibu nyinyi ndio mdomo wa wandishi wa habar, hivyo tunawataka mtoe tarifa wakati kukitokea unyanyasaji kwa wandishi wa habar,” alisema.

Aidha kwa upande mwengine amewataka wandishi wa habari kuielimisha jamii na kufahamu umuhimu wa wandishi wa habari kwani kunaweza kukasaidia kujenga mazingira bora na salama kwa wandishi kufanya kazi zao bila ya vitisho na vikwazo vyovyote.

Kwa upande Mkurugenzi wa Umoja wa Vilabu vya wandishi wa habar Tanzania (UTPC) Kenneth  Simbaya amewataka wandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa kufuata Miko na madili pamoja na kuibua kero za wananchi ili kulinda heshima ya wandishi wa habari.

Mwandishi wa habar kutoka Tanzania bara Marco Maduhu alisema ni vyema kutoa elimu kwa vyombo mbali mbali vya Serikali pamoja na viongozi wa kisiasa kufahamu umuhimu wa vyombo vya habari na wandishi wa habari ili kuona  unyanyasaji kwa wandishi wa habar umeondoka.

Nae mwandishi wa habari ambae pia ni wakili Mveri Mwita amewataka wandishi wa habari kuzisoma na kuzielewa sheria mbali mbali za Nchi jambo ambalo litawasaidia kutekeleza majukumu Yao kwa kujiamini.

Tarehe 2 Novemba kila mwaka kuanzia mwaka 2013, Duniani kote tunaadhimisha Siku ya Kimataifa ya kukomesha Uhalifu Dhidi ya Waandishi wa Habari, (International Day to End Impunity for Crimes against Journalists).

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga dhuluma na ukatili dhidi ya Waandishi wa Habari, UTPC imeendesha Mdahalo kwa njia ya mtandao wa kuwashirikisha wanachama wake ambao ni waandishi wa habari .

MWISHO.