Friday, December 27

SIMBA SC YA KIMATAIFA YAPIGWA TANO NA YANGA SC LIGI KUU

Na.Alex Sonna_Dodoma

YANGA SC imeifanyia mauaji timu ya Simba SC baada ya kuichapa mabao 5_1 Mchezo wa Ligi ya NBC Tanzania bara uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Far es Salaam.

Yanga walikuwa was Kwanza kupata bao dakika ya tatu likifungwa na Kennedy Musonda kabla ya Kibu Denis kusawazisha dakika ya tisa.

Timu zote zilienda mapumziko zikiwa zimefungana bao 1_1.

Kipindi cha pili kilikuwa kibaya zaidi kwa Simba SC wakiruhusu nyavu zao kutikiswa Mara nne.

Timuzote zilifanya mabadiliko kulingana na mahitaji ya Timu Yanga walinufaika na kipindi Cha pili Max Nzengeli alifunga bao la pili dakika ya 64.

Mchezaji Ghali zaidi kwa Yanga Stephanie Azizi Ki alipigilia msumari wa tatu dakika ya 74 kabla ya Max Nzengeli kufunga bao la nne dakika ya 77 likiwa bao lake la pili kwa Mchezo huo.

Kiungaanayewatesa wapinzni kwa Sasa Zouzou Pacome alikamilisha 5G kwa kufunga bao la tano kwa Mkwaju wa Penalti dakika ya 87.

KwaMatokeo hayo Yanga SC wamefikisha alama 21 na kukwea kileleni mwa Msimamo wakiwa wamecheza Mechi name na kuishusha Azam FC nafasi ya pili wakiwa na Alama 19 wamecheza Mechi tisa huku Simba SC wakibaki nafasi Yao ya tatu wakiwa na Pointi 18 wakiwa wamecheza Mechi Saba.