Thursday, January 30

WAANDISHI wa Habari Kisiwani Pemba kupaza sauti zao kusaidia upatikanaji wa haki mbali mbali.

NA AMINA AHMED-PEMBA.
WAANDISHI wa Habari Kisiwani Pemba wameaswa  kupaza sauti zao, katika kusaidia upatikanaji wa haki mbali mbali wanazoendelea kuzikosa watoto wanaofanyiwa udhalilishaji wa kijinsia  kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo, kukosekana kwa sheria maalumu inayosimamia masuala ya udhalilishaji pamoja na  ushahidi madhubuti na kupelekea kufutwa kwa kesi mbali mbali mahakamani kwa kuandika habari  na makala  mbali mbali.
Ameyasema hayo   Mratibu wa chama  cha Waandishi wa Habari TAMWA-Zanzibar kisiwani Pemba Fat-hiya Mussa Said alipokuwa akizungumza na  waandishi wa habari  huko katika ukumbi wa  ofisi hizo  Mkanjuni Chake  chake  katika mafunzo maalum kwa Waandishi juu ya kuandika changamoto zinazowakabili watoto walioathirika na vitendo vya udhalilishaji .
 “Bado  watoto waathirika wa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia wanaendelea kukabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kukosa ushauri nasaha,kukosa fidia zao na kufutwa kwa kesi mbali mbali kutokana na kukosa ushahidi madhubuti  watetezi wa kuzisemea changamoto hizi  waandishi mnayo nafasi kubwa katika kuwasaidia kuzipatia ufumbuzi. “
Akitoa elimu juu ya sheria mbali mbali Siti Habibu Muhammed amesema serikali ya Zanzibar imeanzisha sheria mbali mbali mikataba ya kimataifa pamoja na  mikataba ya kikanda katika kulipatia ufumbuzi suala la udhalilishaji hivyo ni vyema  waandishi hao kuzitumia katika kuasemea mapungufu yanayopelekea kuongeza changamoto na  vitendo vya udhalilishaji kwa waathirika hao.
Nao baadhi ya waandishi wa habari   hao  akiwemo Khadija Kombo wamesema wataendelea kuzisemea changamoto hizo kwa kuandika habari na makaa mbali mbali  zitakazosaidia kuondoa changamoto hizo zinazoendelea kujitokeza kwa waathirika wa udhalilishaji.
Mafunzo hayo maalum yaluoandaliwa na Tamwa kwa Ufadhili wa Faundation for civil Society yamewashirikisha waandishi wa vyombo mbali mbali ikiwemo  Radio, Tv, Magazeti pamoja na mitandao ya  kijamii

Mwisho