Saturday, December 28

Kila anaestahiki anapatiwa elimu ya msaada wakisheria-Hakimu Muumini

 

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA

HAKIMU dhamana wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Muumini Ali Juma, amesema lengo kuu la Wizara ya Katiba, sheria, Utumishi na Utawala Bora, kupitia idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, ni kuhakikisha kila mwananchi anaestahiki anapatiwa elimu msaada wa kisheria.

Alisema bado wananchi waliowengi wanahitaji elimu ya msaada wa kisheri, kutokana na kukumbwa na matatizo mengi na sehemu sahihi ya kupita, ili haki zao waweze kuzipata bado imekua kikwazo kwao.

Hayo aliyaeleza wakati akihairisha mafunzo ya wasaidizi wa sheria, yaliyotolewa na idara ya katiba na msaada wa kisheria Zanzibar na kufanyika mjini Chake Chake, chini ya ufadhili wa UN-Women.

Alisema idara itaendelea kushirikiana ili kuhakikisha Sera na dhamira zinafikiwa, ili kila anaestahiki kupatiwa msaada wa kisheria anapatiwa.

“Watoa msaada wa kisheria hamupaswi kuvunjika moyo, idara inafanya kazi kubwa katika kuwapatia elimu kila sehemu inayostahiki basi elimu inawafikia,”alisema.

Hata hivyo aliwashuhuku UN-Women kwa kuandaa mafunzo hayo, kwani bado elimu inahitajika kwa wasaidizi wa sheria, ikizingatiwa wanafanya kazi kubwa ya kujitolea.

Nae afisa Sheria kutoka Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar Yussra Abdalla Said, aliwataka wasaidizi wa sheria kubadilika kwani fursa wanazozipata wanapaswa kuzitumia ipasavyo, pamoja na kuwashajihisha wenzao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria Wilaya ya Mkoani Nassor Hakim, aliwasihi wasaidizi wa sheria kutokuchoka katika kutoa kwao elimu kwani ipo siku wanaume watajua haki zao na sheria za kadhi.

Aidha nae Msaidizi wa Sheria kutoka Wilaya ya Mkoani Saleh Mussa Alawi, alisema wasaidizi wa sheria ni waathirika wakubwa wa kutokuwepo kwa nyumba za kurekebisha tabia kwa watoto, ikizingatia watoto ni wengi wanaendelea kuathirika.

“kama nyumba ya kurekebisha tabia kwa watoto, basi wale watoto wanaodhalilishwa baadae wangekua na sehemu salama ya kwenda kupata elimu ya saikolojia mpaka akawa sawa,”alise,a

Nae afisa sheria kutoka idara ya katiba na msaada wa kisheria Pemba Bakali Omar Ali, alisema kwa sasa idara inaangalia mafanikio waliopata wa saidizi wa sheria baada ya kupoatiwa mafunzo hayo.

MWISHO