Na Maryam Talib – Pemba.
AFISA Mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mfamau Lali Mfamau amewataka vijana kisiwani Pemba watumie fursa wanazopatiwa na Serikali yao pendwa ya Awamu ya nane ya Dokta Hessein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi kwa lengo la kuleta maendeleo katika nchi.
Aliyasema hayo alipokuwa akizindua rasmi Mafunzo elekezi katika kituo cha Vijana Wete Weni Mkoa wa kaskazini Pemba.
Mdhamin huyo alisema lengo la serikali kuanzinsha vituo hivyo vya mafunzo elekezi vya kusaidia vijana ni kuwataka waondokane na mawimbi ya tabia chafu na badala yake waamke katika kujielimisha katika fani tofauti kwenye vituo vilivoanzishwa kusaidia vijana iliwaweze kujisaidia wenyewe.
Mfamau alisema Rais wa Zanzibar na mwenyekliti wa Baraza la Mapinduzi dk Hussein Mwinyi na wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan wote wamekuwa na Imani kubwa sana kwa vijana wao na hilo linajidhihirisha zaidi kwenye utaratibu wa uongozi uliopo ukiangalia wengi wao ni vijana, hivo amewataka vijana hao kuzitumia fursa vizuri kusudi kuwafanya wale wapendwa wetu wasije wakaondosha Imani hizo.
“Nawataka vijana wetu muchangamkie fursa mulizopewa uzuri wa Serikali hii ya Dokta Mwinyi haina matabaka, yoyote anaweza kuwa kiongozi” alisema Mfamau.
Vile vile aliwataka viongozi wote kwenye maeneo tofauti watekeleze ilani ya chama cha Mapinduzi CCM kama inavoelekeza na kuwataka watumie nafasi zao kwa nafasi zinazojitokeza popote pale zielekezwe zaidi kwenye mahitaji ya vijana kwa lengo la kuwainua kiuchumi,kitamaduni na kisiasa.
Hashir Ali Said ambae ni Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Mkoa wa Kaskazini Pemba akishirikiana na Mwenyekiti wa Umoja wa vijana Mkoa wa Kusini Pemba aliwataka vijana hao kukienzi na kukitunza kituo hicho cha Weni kusudi kiweze kuendelea kuwepo na kuwasaidia wao na hata vizazi vinavofuata.
Nae Mratibu wa Idara ya Maendeleo ya vijana Wizara Habari Vijana Utamaduni na Michezo Ali Mussa Bakar alisema hii ni katika utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025 ambayo inaelekeza vijana hawaachwi nyuma wanapewa vipaumbele kupatiwa mafunzo ya ujuzi na weledi ili kuona na wao hawaachwi nyuma katika kufikia malengo yao.
Alisema vituo hivo vimekuja kwa lengo mahsusi lakuona kila kijana anapata fursa ya mafunzo ya ujuzi na kwa ubunifu na hii ni nia ya dokta Mwinyi ya kueka mazingira wezeshi ya vijana kupata fursa ambayo ipo waweze kupatiwa.
Nae mratibu wa kituo hicho cha Weni Wete Pemba Seif Edward Kabeyu alisema kwa sasa tokea waanzishe mafunzo hayo wamekuwa na jumla ya wanafunzi (61) katika fani tofauti hivyo kuwataka vijana watumie fursa hizo kwa lengo la kujikwamua na baadhi ya mambo ambayo hayaridhishi wasipoteze fursa ambazo wamepatiwa na serikali yao pendwa.
“Niwaambie tu vijana fursa haziji mara nyingi tumieni hivi vituo vyenu kwa kujiengezea ujuzi ambao utawasaidia katika maisha yenu ya baadae” alisema Mratibu wa kituo hicho.
Mwanafunzi wa somo la Urembo Rahma Saleh Salim ambae yupo katika kituo hicho cha Weni alisema wanafuraha kubwa kuanzishiwa vituo hivo vya kuengeza ujuzi kwani hapo zamani ikichukuliwa baadhi ya elimu ni uhuni lakini sasa vijana wamekuwa huru katika kujitafutia maendeleo yao wenyewe.
“Serikali ya Dokta mwinyi kwa kweli ni ya kupigiwa mfano kwani imekuwa ikitoa fursa nyingi kwa vijana jambo ambalo halijawahi kutokea kikamilifu”alisema mwanafunzi huyo.
MWISHO.