Saturday, November 9

Vijana Kisiwani Pemba wametakiwa kuutumia vyema mtandao wa U- Report 

Na Maryam Talib – Pemba.

VIJANA Kisiwani Pemba wametakiwa kuutumia vyema mtando wa U- Report ili kutatua matatizo yao ambayo yangeweza kukuwakwamisha katika kuendeleza maisha yao ya baadae ikiwemo afya ya uzazi, ukimwi na udhalilishaji.

Akitoa maelezo msimamizi wa U- Report  kutoka Wizara ya Habari  vijana utamaduni na michezo Sheila Mwinyi alisema mtandao huu upo kwa lengo la kuwapatia elimu ya kujitambua vijana kusudi kuwaondoa katika majanga ambayo wangeweza kuyasababisha au kusababishiwa wao.

Sheila alisema lengo hasa la kutaka vijana wazitumie fursa wanazopatiwa za kutapa mafunzo yote yanohusiana na mambo yote ya kijamii ni kurekebisha kile kilichotokea huko nyuma kwa wazazi kisije kikatokea  kwao na kupata taifa lililo bora zaidi.

“Vijana nawaombeni sana muzitumie fursa munazozipatiwa kwa kweli Raisi wetu anaona mbali kila fursa anailekeza kwa vijana kusudi kuona taifa linakuwa bora zaidi” alisema Sheila.

Mratibu wa vijana kutoka Wizara ya Habari Vijana Utalii na Michezo Ali Mussa Bakar alisema U- Report inawapa fursa vijana kupata suluhisho la shida zao kwa njia fupi kwani wamewawekea wataalamu wa maswala afya ya uzazi,ukimwi na udhalilishaji  maswala yao yanayowasakili kwa njia ya sms kuuliza maswali na kujibiwa papo hapo.

Alisema vijana ni suala mtambuka ambalo linaingia kila sekta hivyo kuwataka wazitumie vyema fursa wanazopatiwa kwani hawawezi kukua kiuchumi kama fursa hizo hawjazitumia ipasavyo za kupata elimu tofauti kwa mambo yanayowazunguka katika jamii.

Nae Yunuss Mbarouk Kombo ambae ni mratibu wa vijana Wilaya ya Wetealiwaambia vijana hao waondokane na tamaa za pesa kwanza na wajali ni elimu gani wanayotaka kupatiwa kwani fursa zinakuja na kuondoka kama ambayo ujana huishii hapo unaenda kwenye uzee.

Aliwataka vijana hao kisiwani Pemba kuzitumia fursa wanazopatiwa kwani fursa nazo nikama ujana kwendea uzeeni nazo zinatafkia muda zitakuwa hazipo  kama itakuwa umejipatia mapema uzeeni itakuwa ni kutumia tu na kuwapatia wanaokuja.

Nao kati ya washiriki wa umasishwaji wa mafunzo hayo ya Upatikana  ji wa mafunzo ya afya ya uzazi Ukimwi na udhdhalilishaji Rashid Ali Said ambae ni Mwenyekiti wa Club Baraza la Vijana Wete alisema wanayo furaha kubwa kuanzishiwa mtandao huo wa U- Report kwani utawasaidia katika kutatua changamoto zinazowakabili katika kujiletea maendeleo endelevu ya maisha yao.

Aliwataka vijana wenziwe wote waweze kuzitumia fursa hizo vyema na kuwatumia wataalamu ambao wameekea makusudi kuwatatulia shida zao kwanjia ya sms ama mazungumzo ya ana kwa ana kupitia  mtandao huo wa U- Report ambao umewalenga haswa vijana ambao ndio chachu ya maendeleo.

Uhamasishwaji huo mafunzo ya afya ya uzazi,ukimwi na udhalilishaji kwa vijana yamefanika katika Wilaya zote nne Pemba na kuratibiwa na Maafisa wa U- Report wa Wizara ya Habari Vijana Utalii na Michezo Zanzibar.