Sunday, November 24

BIMA ya Jubilee life inathamini mchango wa walimu

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA

MENEJA wa Bima ya Jubilee Life Bertha Magoli, amesema bima hiyo inathamini mchango wa walimu katika suala zima la bima ya maisha, kutokana na umuhimu wa kazi yao ya kufundisha.

Alisema walimu wamekua wakikumbana na changamoto nyingi katika muda wao wote wanapokua skuli, hivyo bima ya Maisha imekuja kumfuta machungu mwalimu pale anapopatwa na tatizo.

Hayo aliyaeleza wakati wa utambulisho wa mdhamini na utoaji wa mada ya kwanza Bima ya Maisha kwa vikundi, wakati mkutano wautoaji wa elimu ya Bima kwa SACCOS ya Walimu Pemba, mkutano uliofanyika Tibirinzi nje kidogo ya Mji wa Chake Chake.

Ailisema bima ya maisha imegawika sehemu mbili, sehemu moja ni bima ya mtu mmoja mmoja, ambapo mwanachama anachukua ulinzi wake mwenyewe.

Bima ya pili ni kikundi, gharama zinakua chini pamoja na uhakikia wa kupata haki ya kuwa unawezako, na kutoa ulinzi kwa majanga ambayo mtu analipwa moja kwa moja.

“Ndugu zanguni walimu sisi Jubilee life tunatambua thamani na mchango wenu, lazima tuwajali walimu wetu ndio maana tumekuja na bima hizi ili muweze kujiunga nazo,”alisema.

Nae Meneja Uhusiano wa Feisal Juma kutoka Jubilee Iife, akiwasilisha mada juu ya bima ya elimu, alisema bila hiyo unachangia kidogo kidogo mwisho wa siku pesa unarudishiwa mwenyeo kwa ajili ya kumsomeshea mtoto wako skuli yoyote unayotaka.

Kwa upande wake meneja wa bima ya afya ya Jubilee Life Swaleh  Abdullhamid Ali, alisema bima hiyo inatoa huduma za wazee kuanzia mika 60 hadi 80 ndio bima inatambua.

Mapema naibu kamishna wa TIRA Khadija Issa Said, alisema bima ni huduma inayolinda ajali na athari mbali mbali ambazo humtokezea, hivyo bina inauwezo wa kulipa baada ya taratibu kukamilika.

“Tumekua tunasisitiza wateja wetu kuhakikisha wanakata bima katika maeneo sahihi ambayo pale mtu anapopatwa na tatizo unaweza kupata fidia yako baada ya taratibu kukamilika,”alisema.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, aliwataka wanaSACCOS ya Walimu, kuhakikisha wanakata bima kwa manufaa yao, ili wapopata na tataizo itakua rahisi kusaidiana.

Akitoa neno la shukuran Mwenyekiti wa SACOOS ya walimu Said Suleiman, aliishukuru TIRA kwa kufika na kutoa elimu hiyo kwa walimu juu ya umuhimu wa bima hiyo.

MWISHO