Saturday, December 28

HABARI PICHA: Bonanza maalumu la kuelelea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.

MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali(mwenye flana nyekundu), akiwaongoza Viongozi mbali mbali wa Taasisi ya ZAYADESA katika bonanza maalumu la kuelelea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, kitaifa mwaka huu yanafanyika Kisiwani Unguja
Mratibu Tume ya Ukimwi Pemba Ali Mbarouk Omar, akizungumza katika bonanza lililoshirikisha michezo mbali mbali na kuandaliwa na Taasisi ya ZAYADESA huko katika viwanja vya Gombani, ikiwa ni kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani
MKURUGENZI Mwendeshaji wa Taasisi ya ZAYADESA Dk.Mahmoud Mussa, akitoa malengo ya bonanza hilo lililoshirikisha vyuo vikuu, ikiwa ni kuelekea siku ya Ukimwi Duninia, huko katika viwanja vya Gombani Kongwe Wilaya ya Chake Chake
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, akizungumza na vijana kutoka vyuo vikuu mbali mbali Pemba, ambavyo vimeshiriki katika bonanza maalumu la kuelekea kilele siku ya Ukimwi Duniani, huko katika viwanja vya Gombani Kongwe Wilaya ya Chake Chake
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, akipiga Penant kuashiri uzinduzi wa bonanza la michezo mbali mbali ya Vyuo Vikuu, iliyoandaliwa na taasisi ya ZAYADESA nakufanyika Gombani Mjini Chake Chake.

 

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)