Thursday, January 30

TAKWIMU ZA UDHALILISHAJI KWA MWEZI WA OKTOBA 2023


Jumla ya matukio 199 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa kwa mwezi wa Oktoba 2023, yakiwa na idadi 199 ya waathirika wa matukio hayo, ambapo waathirika wengi wakiwa ni Watoto kwa asilimia 78.9, wanawake 16.1 na wanaume asilimia 5.0.
akitoa takwimu hizo Mtakwimu kutoka Divisheni ya Jinsia na ajira katika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar Ndugu Ramla Hassana Pandu amesema idadi hiyo ya matukio 199 kwa mwezi wa Oktoba ni ongezeka la asilimia 26.8 kutoka matukio 157 yaliyoripotiwa mwezi wa Septemba 2023.
Ndugu Ramla akitoa mlinganisho wa makossa hayo kwa wa septemba na Oktoba 2023 amesema, matukio ya kubaka kwa mwezi wa Septemba yalikua 59 ambapo kwa mwezi wa Oktoba yamefikia 89, ikiwa ni ongezeka la makossa 30, makossa ya kulawiti na kunajisi septemba yalikua 15 Oktoba 22, makossa ya kuingilia kinyume na maumbile Septemba yalikua 6 Oktoba 13, kutorosha Septemba makosa 11na Oktoba makosa 10.
Aidha makosa ya shambulio la aibu au kukashifu kwa mwezi wa Septemba yalikua 24 Oktoba makossa 22 na kwa upande wa makossa ya shambulio kwa mwezi wa Septemba yalikua 42 ila kwa mwezi wa Oktoba yameongezekamna kufikia 43. idadi ya matukio hayo 199 kwa Oktoba 2023, yameongezeka kwa asilimia 21.3 kutoka matukio 164 yaliyoripotiwa mwezi Oktoba 2022.
Akizitaja Wilaya zinazoongoza kwa matukio ya ukatili na udhalilishaji amesema kuwa Wilaya ya Mjini na Wilaya Magharibi ‘B’ zimeripotiwa kuwa na matukio mengi zikilinganishwa na wilaya nyengine kwa matukio 52 sawa na asilimia 26.1 kwa kila wilaya. ikifuatiwa na Wilaya ya Magharibi A’ yenye matukio 37 sawa na asilimia 18.6, Wilaya za Micheweni na Mkoani zimeripotiwa kuwa na idadi ndogo ya matukio ya uidhalilishaji kwa kuwa na matukio matatu 3 sawa na asilimia 1. 5 kwa kila wilaya.
Aidha amesema Wilaya ya Mjini imeripotiwa kuwa na idadi kubwa ya matukio ya kubaka ikilinganishwa na wilaya nyengine kwa matukio 22 sawa na asilimia 24.7 kati ya matukioa yote ya kubaka yaliyoripotiwa, ikifuatiwa na Wilaya ya Magharibi B kwa matukio ya ubakaji 19 sawa na asilimia 21.3.
Kati ya matukio 89 ya ubakaji yaliyoripotiwa kwa mwezi wa oktoba 2023, matukio 15 sawa na asilimia 16.9 yameripotiwa kwa wanawake na matukio 74 yameripotiwa kwa wasichana sawa na asilimia 83.1
akitaja hatua zilizochukuliwa amesema kuwa kati ya matukio yote 199, matukio 139 yapo chini ya upelelezi wa jeshi la polisi sawa na asilimia 69.9, matukio 57 sawa asilimia 28.6 yapo Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na matukio matatu 3 sawa na asilimia 1.5 yapo mahakamani

Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano,
Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali,
Zanzibar.