Sunday, December 22

HABARI PICHA: Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, atimiza ahadi yake kwa Timu ya Karume Boys ya Zanzibar.

 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, akabidhi kiasi cha Shilingi Milion mbili na Laki Tano kwa Waziri Habari, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita, akitekeleza ahadi yake kwa Timu ya Karume Boys ya Zanzibar chini ya miaka 15, ya kununua kila goli litakalofungwa katika mchezo wa Fainali ya CECAFA U-15, kati yao na wenyeji Uganda. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Novemba 22, 2023 ofisini kwake Migombani Mjini Zanzibar. Kitengo cha Habar Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Novemba 22, 2023.