Sunday, December 22

Uongozi wa chuo cha mafunzo ya Amali Vitongoji waametakiwa kushirikiana kamati ya ushauri ya chuo hicho.

Na Thureya Ghalib – PEMBA.   

Uongozi wa Chuo cha amali vitongoji umetakiwa kutoa mashirikiano kwa Kamati ya ushauri wa Chuo hicho katika kufanya mamuzi sahihi na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili .

Wito huo umetolewa Mratibu wa chuo cha mafunzo ya amali Pemba Othaman Said Othaman Kwa niaba ya Ofisa Mdhamini Wizara ya Elimu Na mafunzo ya mali katika uzinduzi wa Kamati  hio  Vitongoji Wilaya ya Chake Mkoa wa Kusini Pemba

Alisema ni vyema Kamati hio wakaitumia  vizuri kwa kupokea na kusikiliza  ushauri utakaojadiliwa katika vikao vya kamati hio  na kuifanyia kazi katika  kuleta mafanikio na kukisogeza mbele chuo hicho .

“Kutokana na Nafasi zenu mulizonazo nina uhakika muna uwezo mkubwa wa kusaidia  kutatua changamoto na kufanya maamuzi yaliyo sahihi ” Alisema Mratibu huyo .

Aidha ametoa pongezi kwa wale wote waliochangia katika kuanzishwa mamlaka, sheria na miongozo mpka kufikia kundwa kwa kamati hiyo  pamoja na  viongozi waliosaini sheria ya kuanzishwa kwake .

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kamati hio ambae ni Afisa mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na michezo Pemba Mfamau Lali Mfamau aliomba Kamati hio kushirikiana kwa hali na mali ilikufanikisha malengo ya kuundwa kwa Kamati hio.

Aidha alifahamisha kuwa katika kutekeleza majukumu yao kutatokea changamoto ndogondogo inabidi wazivumilie  ili kuona kamati inatendewa  haki  na kuona maendeleo ya vyuo vyetu hivi.

“Hili jukumu halina mwenyewe ,hili nijukumu letu sote ,panapotekelezeka basi tumetekeleza sote na panapoharibika tumeharibu sote sasa jukumu letu nikushirikiana kwa hali na mali ili kuona hili gurudumu tulilopewa tunalipeleka mbele”Alisema Mfamau.

Aidha Mfamau aliwaomba walimu wa skuli hio kuhakikisha wanawasomesha wanafunzi  kwa ujuzi na  weledi  wa hali ya juu ili kuona wanafunzi wanaomaliza chuoni hapo wataleta   tija na kukitangaza chuo chao Kwa ujuzi wao mzuri.

Kwa upande wao wajumbe wa kamati hio wameahidi kutoa mashirikiano yao ya dhati na kamati yao na kuahidi watakuwa pamoja katika kuzitafuta na kuzitatua changamoto zinazozikumba chuo hicho.

Kamati hio ya Ushauri lengo lake kuu ni kukishauri chuo katika kukisogeza mbele na imewashirikisha wajumbe mbalimbali akiwemo Mwenyekiti amabaye ni Afisa Mdhamini Wizara ya habari ,Sheha wa shehia ya kibokoni ,Afisa Elimu Wilaya ,Kamanada wa Polisi Wilaya na chake ,Rais wa Serikali ya wanavunzi wa chuo hicho na Walimu.

        Mwisho.