Monday, January 27

POLISI KUZUWIA UHALIFU KIDIGITALI

NA OMAR HASSAN – ZANZIBAR 

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. HAMAD KHAMIS HAMAD amesema Utendaji wa kusimamia Sheria wa Jeshi la Polisi lazima ubadilike kwa kujikita katika matumizi ya taaluma na vifaa vya kisasa ili kukabiliana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanaoendana na mabadiliko ya ufanyaji wa uhalifu.

Akifungua mafunzo ya Mfumo wa kutoa taarifa kidigitali, kwa Wakaguzi wa Shehia Mikoa ya Zanzibar, hapa Ukumbi wa Chuo cha Polisi Zanzibar amesema mafunzo hayo yatarahisisha upatikanaji wa taarifa za uhalifu haraka na kufanyiwa kazi kwa wakati.

Nae Mrakibu wa Polisi Kutoka Makao Makuu ya Polisi Dodoma DKT. EZEKIEL KYOGO ameeleza kuwa Matumizi ya Technolojia kwa Watendaji wa Jeshi laPolisi ni muhimu na yatasaidia kutoa huduma bora za kipolisi kwa wananchi.

ALI SHAIBU mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP amesema Shirika hilo linasaidia Mafunzo na Vifaa kwa Jeshi la Polisi ili kuzuwia uhalifu na kuendeleza Amani nchini Tanzania.

Pamoja na Mafunzo hayo pia Shirika la UNDP pia limesaidia vifaa vya mawasiliano vikiwemo Komputa pamoja na simu vitakavyotumika kukusanya taarifa katika Shehia mbalimbali.