NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuandaa mifumo imara mifumo ambayo itaweza kusaidia utaratibu mzima wa ulipaji wakodi kwa mtu husika.Alisema kuwepo kwa mfumo hiyo itasaidia kuongeza tija katika suala zima la ulipaji wakodi, pamoja na udhibiti wa miaya ya upotevu wakodi hizo.
Akizungumza kwa niaba yake Mkuu wa Wilaya ya Wete, Dr Hamad Omar Bakar, wakati wahfla ya ufunguzi wa Ofisi ya Wete kikodi ya TRA, ikiwa ni Wiki ya Shukurani kwa walipakodi Pemba, ilioambatana na kauli mbiu “Kodi Yetu, Maendeleo Yetu, Tuwajibike” nakufanyika Mtemani Wete.
Aidha mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wananchi kutumia mfumo wa kieletroniki wakati kukusanya mapato, pamoja na kuhakikisha wanadai risiti zakieletroniki.
“Katika hizi kazi zetu lazima tutangulize suala zima la uzalendo hapo wananchi na wafanyabiashara wataweza kulipa kodi zao ipasavyo,”alisema.Hata hivyo Mkuu huyo alisema suala la ulipaji wakodi ni jambo la muhimu sana, kwa sababu kuna mahusiano makubwa baina ya walipa kodi na huduma zianzotolewa ndani ya nchi.
“Hakuna mwananchi ambae hapendi miundombinu mizuri, barabara, umeme, maji, elimu hakuna mwananchi ambae hataki huduma za kijamii,”alisema.Alisema uchumi wa Zanzibar hauwezi kufikia bila ya kuwepo kwa kodi na usuhuru, kwani hakuna nchi yoyote dunaini inayensgwa pasinamisingi ya ulipaji wakodi.
Akizungumzia suala la ufunguzi wa Ofisi, alisema ni kusogeza huduma karibu na kutarahisisha walipakodi kulipa kwa wakati tafauti na kufuata huduma Chake Chake.
Mapema akimuwakilisha Kamishna Mkuu wa TRA Tanzania, kaimu Naibu Kamishna wa Huduma za Kiufundi Venance Mshana, alisema wanatekeleza mikakati mbali mbali, ikiwemo kuboresha mifumo ya tehama ili kurahisisha suala zima la ulipaji wakodi, pamoja na kusogeza huduma karibu zaidi kwa walipa kodi kwa Wilaya ya Wete.
Aidha alisema suala la ukusanyaji wamapato kwa katika mkoa wa Pemba yanaendela vizuri, ambapo ufunguzi wa ofisi hiyo Wilaya ya Wete itaqweza kuwafikia walipakodi wengi kwa kuwasajili na waliokua bado ili kuingiza katika wigo wa ulipaji wakodi.
Nae Meneja TRA Pemba Arif Maohamed Said, alisema wananchi wanafursa nzuri ya kupata huduma hizo, pamoja na kuchangia maendeleo ya nchi yao kupitia kodi.
Akizungumzia dhamira ya kufungua ofisi Wete ya kikodi, ni maalumu ambayo TRA walikua nayo ili kusogeza huduma karibu na wananchi, ili kulipa kodi bila ya kusumbuka, ikizingatiwa walipajikodi wengi ni wafanyabiashara na sio busara maduka kufungwa wakati maeneo yapo.
MWISHO