Saturday, December 28

Jumla ya Miradi 23 kusini Pemba inatarajiwa kufikiwa kuelekea kilele cha Sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar.

Na Thureya Ghalib ,Pemba.

Jumla ya Miradi 23 inatarajiwa kufunguliwa kuzinduiwa pamoja  na kuekewa mawe ya msingi katika Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni shamra shamra za kuekelea kilele cha Sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar .

Hayo yamelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari huko ofisini kwake Wilaya ya Chake Mkoa wa Kusini Pemba.

Mattar amesema miradi 10 itafunguliwa katika Mkoa huo ,miradi 4 itazinduliwa na miradi  9 itaekewa mawe ya msingi ,ambayo inahusu masuala ya maendeleo ya Wananchi .

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Wananchi kushirikiana katika shughuli zote ,kwani sherehe hizo hasihusiani na masuala ya kisiasa au itikadi zozote.

Pamoja na hayo ametoa Wito kwa Wananchi kushiriki katika shughuli za Usafi hapo Kesho ,kwani Usafi ni Afya na unaondosha Maradhi mbalimbali.

Mwisho