Na Maryam Talib – Pemba.
Ofisa Mdhamin Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba Mfamau Lali Mfamau amewataka baadhi ya vijana kisiwani Pemba kuibua na kuuchangia vyema Mpango mkakati wa kitaifa katika vipengele vyote ambavyo vimeainishwa katika mpango huo utakaowasilishwa na washauri elekezi wa mpango huo.
Aliyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo yaliyoendeshwa kwa siku mbili yaliyowashirikisha vijana wenye mahitaji maalumu , vijana wa mitaani , vijana walio sober house, na kundi la wanasiasa kutoka maeneo tofauti ya kisiwa cha Pemba katika ukumbi wa Wizara ya fedha na ukumbi wa Makonyo Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba.
Mdhamini huyo aliwaambia vijana hao hiyo ni fursa ya kipekee ambayo wamepatiwa hivyo kutoa michango iliyo bora ili iweze kuleta matokeo halisi ya maoni ambayo wameyatowa vijana wenyewe katika michango yao.
“Nawambia vijana kwakweli ni jambo la kujivunia fursa hizi kwani mafunzo haya yameanzia Pemba na baadae yataelekwa Unguja” alisema Mdhamini huyo.
Aliwaomba vijana hao kuipitia sera yao ya mwaka 2023 ilizinduliwa punde tu kwani ndio itayowaelekeza mambo yao yote katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Mshauri elekezi wa utayarishaji wa mkakati wa Kitaifa wa Vijana Kimwaga Muhidini alisema katika kutengeneza mkakati huo utazingatia zaidi kwenye sera ya vijana, mawazo ya vijana, hati za kitaifa na mkakati wa kitaifa, umoja wa afrika wataangalia huko vijana wamezungumzaje, malengo ya maendeleo endelevu (SDG) pia yanasemaje kuhusiana na vijana.
Mshauri huyo elekezi alisema Serikali imeona mbali sana na ndio mana kila hatua ya utekelezaji imekuwa ikiwagusa vijana kwani kumekuwa na ongezeko kubwa la vijana hao kwani ndio wahanga wa majanga tofauti na mazingira yao yamekuwa yakitoutisha katika upatikanaji wa fursa ambazo zinajitokeza.
“Kiukweli mara nyingi vijana walioko mjini tofauti na walioko kijijini katika upatikanaji wa fursa za kujiendeleza kimaisha na hata takwimu zinaonesha uhalisia wake.”alisema Kimwaga.
Alisema lengo mahasusi la kufanya mafunzo hayo ya ukusanyaji wa mawazo na changamoto za vijanana kuona hali halisi ya maendeleo ya vijana yapo wapi, yanaelekea wapi na yatafikwaje mwisho wa yote hayo ni kuweka mfumo maalumu wa ufuatiliaji na tathmini ili kuona lile lengo limefikiwa kama lilivokusudiwa.
Nae mchangiaji katika mafunzo hayo ambae ni Afisa Elimu Chake Ckake Burhani Khamis Juma alisema wakati wa kuchukua maoni na changamoto kama hizo ipo haja ya kuchanganya vijana hususani walio mitaani kwani wao ndio walio katika majanga zaidi na sio walio katika sekta za vijana kuwawakilisha wao tu.
kwa upande wake katibu wa UVCCM Wilaya Chake Chake Ibrahim Saleh Issa amesema vijana ipo haja kuwa mabalozi wema kwenye fursa zote zinazopatikana kwani kila mafunzo au kuchangia mawazo haiwezekani kuingia vijana wote hivyo ipo haja ya wale wanaopata nafasi ya kuhudhuria chochote kinachohusu kijana kukipeleka kwa vijana wengine waliowazunguka.
“kiukweli mimi binafsi nilihudhuria mfunzo mara mbili ya kuhusiana na uundwaji wa sera ya vijana ambayo imezinduliwa punde ya mwaka 2023” alisema Katibu huyo
Nae maratibu wa vijana kutoka Wizara ya Hbari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba Ali Mussa aliwaasa vijana hao waliopata fursa ya kutoa michango katika mafunzo hayo wayachukue vyema na wakayatumie kwa vijana wenzao ili waweze hata kuchangia baadae.
Mwisho.