Saturday, December 28

Vijana wametakiwa kutambua vyema kinachoendelea katika masuala kusimamisha Utawalaa bora 

 

 

Na Maryam Talib – Pemba. 

Ofisa Mdhamin Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Pemba Halima Khamis Ali aliwataka vijana kutambua vyema kinachoendelea katika masuala kusimamisha Utawalaa bora  katika maeneo tofauti  kwani vijana ndio nguvu kazi ya taifa kusudi kuwa mabalozi wazuri katika jamii zetu.

Aliyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa siku moja uliowashirikisha vijana 40 kutoka shehia tofauti za Wilaya Chake Chake uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala bora kisiwani Pemba.

Mdhamin  huyo alisema mafunzo hayo ya Rshwa na utawala bora ,ajira  yamefanyika kwa vijana kwani wao ndio wahusika katika maswala  mengi vijana kwani taifa imara ni taifa lenye vijana wengi lakini  wawe na uzalendo  na uchungu wa nchi yao.

Alisema utawala uzalendo sio nyimbo wala kupiga kofi uzalendo ni kuiyona changamoto iko wapi kusimama na kupigania taifa ili nchi isizame hivyo utawala bora unakufanya kujielewa na kujifahamu.

“Tumewaiteni hapa vijana kuwafunza maswala ya utapeli katika ajira  (Rushwa) ili muwe mabalozi kwanda kupambania kwani kuna jamii zinalalamikiwa na kulalamika kwenye sula hili mukaifanye kazi”alisema mdhamin.

Alisema ipo haja kama vijana kupambana na kuipambania katika kufikisha ujumbe kwa lengo la kuisaidia jamii ili haki ipatikane kwani haki hainunuliwi haki ya ajira hiyuzwi wala haina  dalali kwani yote hayo yana utaratibu wake.

Akitoa maelezo mafupi katika mafunzo hayo Mratibu Idara ya Uwala Bora Pemba Mohamed Masoud Said alisema kuwambiaa vijana hao kwamba Utawala Bora ni Neno mtambuka ni neon ambalo linaigia kila pahali linajumuisha Uwazi ,ushirikishwaji,utawala wa sharia na nyenginezo.

Alisema kama vijana munatakiwa kuufahamu kwa kwa kina kwa kila hatua kusudi kuweza kutatua mambo yenu katika shuhuli zinazowazunguka katika jamii.

 

Nae mtoa mada kutoka tume ya utumishi serikalini Pemba Omar Khatib Ngwali alisema kwa sasa serikali imejipanga vizuri kwani maombi yote ya ajira yamekuwa kwenye utaratibu wa mfumo na sio kwa makaratasi kama ilivozoeleka zamani hii yote ni kuondosha utapeli katika maswala hayo ya ajira.

“Nawaomba vijana mulichukue vyeli mukasaidie vijana wenzenu huko katika jamii mana nyinyi ndio wahanga wakuu wa majanga haya”Alisema Omar.

Nae Mchangiaji katika mafunzo hayo ambae ni Mwenyekiti wa vijana Wilaya ya Chake Zuleikha Maulid Kheri alisema ipo haja ya kuyaendeleza mafunzo hayo kwa hali yoyote kwani hali bado ni tete hususana katika upatikanaji wa ajira kwa vijana.

“Mimi naona ni wakati sahihi sasa kama vijana kwenda kuineza elimu hii katika jamii zetu kwani tumeshaumizwa sana “alisema Zuleikha.

Mwenyekiti huyo alisema mafunzo hayo rushwa katika ajira yamekuja katika kipindi sahihi  kwa upande wao ili wasiweze kuingia katika rushwa na kuzidi kudumaa kiuchumi kwani mafunzo yamekuja kuwaokoa vijana hao .

MWISHO.