Tuesday, November 12

Wamiliki wa vyombo vya habari wametakiwa kujisajili Tume ya Utangazaji.

 

Na Maryam Talib – Pemba. 

Ofisa Mdhamin Wizara ya habari Vijana Utamaduni na Michezo Mfamau Lali Mfamau amewataka wamiliki wa vyombo vya habari hususani  online tv wasajili vyombo vyao  Tume ya utangazaji kwa lengo la kuondosha shubha ama changamoto  zinazojitokeza katika kazi zao.

Aliyasema hayo alipokuwa akifungua mapitio ya sheria ya tume utangazaji yaliyofanyika katika ukumbi wa uwezeshaji Gombani Kisiwani Pemba

Mdhamini huyo alisema lengo la kufanya hivyo ni kuona vyombo vyote vinatoa taarifa zake kwa jamii iwe zinaendana na mazingira ya watu na endapo itatokezea  tatizo kwenye taarifa iwe ni wepesi kuelekezana na kurudi kwenye mstari kwani kila binadamu ana mapungufu yake.

“Na nyinyi watu wa tume nawambia iwe basi mana kuna watu wengine wanadharau kuvunja utaratibu kwa makusudi anaekataa naomba sheria ichukue mkondo wake.”alisema Mdhamini.

Aliwataka wadau wa mkutano huo kutoa michango mizuri kwani fursa imekuja inatakiwa kutumiwa ipasavyo kwa kusajili na kutafuta vitambulisho vinavotambulika na Serikali na viongozi wa sekta nyengine zote zitowe msaada kwenye hili.

Nae Katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji wa Zanzibar Suleiman Addulla Salim alisema walifanya hivyo kwa makusudi kwa sababu ya kuona hali inavyoenda kwa sasa sio salama  na ndio maana wameona ipo haja kuzungumza na vyombo vya  habari hususani  vyombo mtandaoni  ili kusudi kuona ni njia gani itakuwa nyepesi zaidi ya kusaidiana kwani sio salama kwa nchi yetu katika suala zima la utamaduni na pia katika kuiunganisha jamii.

Alisema unapoendesha utangazaji usiokuwa na leseni ni kinyume na sheria ifike pahala vyombo vyote vye vya habari visajiliwe kwa lengo pia la kuipatia serikali taarifa sahihi na pia kupatikana kwa fursa zinazoweza kujitokeza.

Nae Afisa Sheria  Tume ya utangazaji Khadija Mabrouk Hassan alisema alipokuwa akiptia sheria ya utangazaji ya Na.7 ya  mwaka 1997 ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka 2010 alisema  bado sheria hiyo ingalie na mapungufu.

Alisema ni vyema sheria hiyo ikafanyiwa marekebisho ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia habari kama tunavojua kwamba teknolojia ya habari na mawasiliano duniani inabadilika mara kwa mara kwa lengo la kutaka mabadiliko ya sheria ni  kuhakikisha kulinda mila silka na tamaduni na amani ya nchi.

“Tunataka tukidhi vigezo katika sheria yetu ili tuendane na mabadiliko ya sayansi na Teknolojia”  Alisema Mwanasheria.

Nae Mchangiaji katika mapitio ya sheria hiyo ya Tume ya utangazaji Zanzibar Nassor Suleiman Nassor alisema ipo haja mabadiliko hayo sheria yakazingatia na makundi ya  mahitaji maalum katika utekelezaji wa sheria hizo kwani wapo walio na uwezo kwa mujibu wa hitajio lake.

Nae mchangiaji mwengine kutoka Juu Media Ummulkulthum Ali Bakar alisema katika sheria hiyo itakayorekebishwa ipo haja ya kuanzia diploma na sio degree kwani hata alie na diploma anaweza akafanya vitu vikubwa zaid ilimradi iwe sifa inamruhusu.

Akitoa neno la shukran Mrajis Tume ya utangazaji Zanzibar Mohamed Said Mohamed  alisema  wameipokea michango yote iliyotelewa na wadau na wataifanyia kazi ipasvyo na ameomba  ushirikiano kwa wadau hao kwani wote wapo katika jahazi moja.

 

 

MWISHO.