YOTE HII NI KASI YA DR. MWINYI ,BONANZA LA MICHEZO LINAWEZEKANA.
Na Maryam Taalib – -Pemba.
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid amewataka watendaji wa Taasisi pamoja na wananchi kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuimarisha afya zao kupitia michezo tofauti ili kuondokana na kupata maradhi hatarishi.
Ameyasema hayo wakati akizindua Bonanza la michezo katika uwanja wa Gombani Kongwe Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni katika heka heka za kusherehekea kwa kutimiza miaka (60) ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Alisema amefarajika kwa kiasi kikubwa kuona wanataasisi wamejitokeza kwa wingi katika mashindo hayo ya michezo tofauti tofauti.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya alimpongeza Ofisa Mdhamini Wizra ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba Mfamau Lali Mfamau kwa kuwa mbunifu mzuri wa kuzinsha Bonanza hilo ikiwemo michezo ya wanawake.
“Nawaombeni wana taasisi na wananchi kwa ujumba huu ni mwanzo mzuri ambao tunaenda nao tunatakiwa tuwe tunacheza hii michezo kila baada ya muda na sio tusubirie kila ifikapo kusherehekea sherehe za Mapinduzi kama tulivojizowesha.”alisema Rashid
Kwa upande wake Afisa mdhamini Wizara ya habari Vijana Utamaduni na Michezo Mfamau Lali Mfamau alisema Mapinduzi yamekuja kumkomboa mwananchi na hii inaonekana kwa anaefahamu tulipotoka ,tulipo na tunakoelekea, haya yote na mengineo ni hatua kubwa ya maendeleo katika nchi yetu.
Mfamau alisema amefurahishwa sana kwa kuona ushiriki mkubwa wa wanawake kwa kushiriki na kushindana katika michezo tofauti katika Bonanza hilo la kusherehekea kuelekea miaka (60) ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Mchezaji mwanamke kutoka Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Nd, Hamisa Omar Hamad aliweza kunyakua ushindi wa kufukuza kuku pamoja na ushindani wa kukuna nazi katika Bonanza hilo.
“Kwa kweli michezo tunahitaji kuiendeleza mara kwa mara kama Mdhamini alivyotuanzishia kwenye washindani wengi ushindi ni jambo zito leo tumejinyakulia Wizara ya habari mashindani ”alisema Hamisa.
Tasisi Kumi na moja za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kisiwani Pemba ambazo zimeingia katika mashindano hayo ya kusherekea Miaka (60) ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
MWISHO.