Friday, January 10

Waziri Dkt.Khalid aweka jiwe la msingi hanga la askari wa Zimamoto na Uokozi Finya.

 

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA 

WAZIRI wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt.Khalid Salum Moh’d, amesema kikosi cha Zimamoto na uokozi ni muhimu sana nchini na duniani kote, na vinapewa haeshama kubwa kutokana na kukabiliana  na majanga mbali mbali ikiwemo ya kimaumbile na yasio kua ya kimaumbile.

Alisema serikali ya Mpainduzi ya Zanzibar nayo imeamua kukipa heshima kubwa kikosi hicho, kutokana na kazi zao nzuri na ngumu wanazozitoa za uokozi.

Waziri Dkt.Khalid aliyasema hayo wakati alipokua akizungumza na wananchi, askari wa Vikosi vya ulinzi na usalama, mara baada ya kuzindua na kuweka jiwe la msingi Hanga la askari wa kikosi hicho.

“Wanafanyakazi kubwa kwenda kuoa watu au mali pale panapotokea majanga yoyote, wanakila sababu ya kupewa msaada unaostahiki kutokana na kazi hizo”alisema.

Aidha alisema serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Dkt.Hussein Ali Mwinyi, inafanya kazi kubwa ya kuhakikisha inakiimarisha na usahihi ni haya majengo yao ya kisasa yanayojengwa.

Hata hivyo alisema serikali inafanya juhudi kubwa ili kuhakikisha vifaa stahiki kwa ajili ya jeshi hilo vinapatikana, ambavyo vitaendana na maendeleo ya ukuaji wa uchumi wan chi kwa sasa.

Alifahamisha kwamba kunauwekezaji katika visiwa vidogovidogo, serikali itajitahidi kuhakikisha kuna kua na vifaa vya kuweza kutoa huduma za uokozi katika maeneo ya visiwa.

“Zipo boti ambazo zinaweza kupambana na moto katika bahari, tunaendelea kuangalia uwezekana wa kuwa na herekpota kwa kusaidia huduma za uongozi yanapotokea majanga baharini,”alisema.

Aidha aliwataka wananchi kujiandaa pale wanapojenga majengo kuhakikisha wanaweka vifaa vinavyoweza kuepusha majanga, pamoja na kuhamasika kukata bima ya mali na majengo yaetu.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, akitoa salamu za wananchi wa Mkoa huo, alisema marehemu Hayati Mzee Abeid Amani Karume alianzisha suala zima la ulinzi na usalama katika nchi baada ya kupatikana kwa mapinduzi yam waka 1964.

Kwa upande wake Kamishna wa Zimamoto na Uokizi Zanzibar Rashid Mzee Abdalla, alimshukuru Rais Dkt.Husseina Ali Mwinyi, kwa kuwapatia fedha na kujenga hanga la askari wa Zimamoto na Uokozi, kwani muda mrefu askari hao walikua na tatizo la malazi.

“Wengine walikua wanalala humo humo katika eneo dogo wanalofanya kazi, wengine wakilala mitaani lakini hali ya kipato ilikua hairuhusu na chakufanya hawana,”alisema.

Mapema naibu Katibu Tawala za Mikoa Zanzibar Mikadadi Mbarouk Mzee, alisema jengo la hanga la askari hao ambapo gharama lilipangiwa kutumia Milioni 250 hadi kukamilika kwake limetumia Milioni 230 fedha kutoka Serikalin.

Aidha alisema jengo la nyumba za kulala maafisa limepangwa kutumia Jumla ya Bilioni 1.1 ambapo hadi sasa limeshatumia shuilingi 330, ambapo mafundi ni kutoka ndani ya kikosi hicho cha zimamoto.

Alisema kukamilika kwa majengo hayo kutaongeza ufanisi wa kiutendaji wa kikosi cha zimamoto na uokozi na kuondosha changamoto iliokua ikiwakabili ya kukosa makazi bora.

MWISHO