NA KHADIJA KOMBO – PEMBA
Benki kuu ya Tanzania BOT imewaomba Viongozi wa Dini pamoja na washereheshaji katika sherehe mbali mbali kutumia nafasi zao katika kuwaelimisha wananchi juu ya kutunza fedha ili kuepusha hasara ya kutengeneza sarafu hizo mara kwa mara.
Wito huo umetolewa na Meneja Msaidizi Kitengo cha Sarafu Benki Kuu makao makuu madogo Zanzibar Suleiman Khalfan Rajab huko katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Chake Chake wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Dini pamoja na washereheshaji (MC) katika shughuli mbali mbali Kisiwani Pemba juu ya namna ya kutunza fedha pamoja na kuzitambua alama muhimu zilizomo katika noti ili kuzifahamu noti bandia.
amesema hivi sasa wananchi wamekuwa na mtindo wa kuharibu fedha kwa makusudi hasa wakati wa kutunza katika sherehe mbali mbali kwa kuzitoboa au kugandisha kwa gundi jambo ambalo husababisha hasara kubwa kwa serikali.
Aidha amewataka wananchi kuepuka kuharibu wa fedha kwa makusudi kwani hilo ni kosa la jinai na atakaye bainika haitosita kushukuliwa hatua.
Akizungumzia kuhusu fedha bandia amewataka wananchi kuchukua tahadhari juu ya kuzitambua alama za noti halali ili kuepuka kupokea noti bandia ambazo zitawatia hatiani.
Kwa Upande wao washiriki wa Mkutano huo wameishukuru BOT kwa kuwapatia elimu hio hivyo wameaahidi kuifikisha kwa jamii ili kuepuka madhara na hasara inayoweza kutokea.
angali video hii kwa kubofya hapo chini
MWISHO.