Thursday, December 26

HABARI PICHA: Uwekaji wa jiwe la msingi kiwanda cha kusarifu mwani Chamanangwe.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi, akipata maelezo ya ujenzi wa kiwanda cha kusarifu mwani Chamanangwe, kutoka kwa mkuu wa KMKM Zanzibar Kamanda Azan Hassan Msingiri, mara baada ya kuwasili katika kiwanda hicho, ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi, akikujua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi Kiwanda cha kusarifia Mwani Pemba, kushoto ni Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar OmAR Said Shaaban, ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi, akipata maelezo kutoka kwa injinia wa wakala wa majengo Pemba Said Maliki, juu ya kiwanda cha kusarifu mwani Chamanangwe, ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban, akimueleza jambo Rais alipokua akikagua kiwanda hicho mara baada ya kuweka jiwe la msingi, ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi, akieleza jambo wakati alipokua akikagua kiwanda cha kusarifia Mwani Chamanangwe, mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi, akitoka kukagua kiwanda cha kusarifia Mwani Chamanangwe Pemba, akiwa na viongozi mbali mbali wa serikali Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete, mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi kiwanda cha kusarifia Mwani Pemba, ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar
WAZIRI wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban, akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi Kiwanda cha kusarifia Mwani Chamanangwe Wilaya ya Wete, ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar
MBUNGE wa Jimbo la Kojani, pia ni Naibu Wazairi wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hamad Hassan Chande, akitoa salamu za wananchi wa Kojani, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kiwanda cha kusarifia Mwani Chamanangwe Wilaya ya Wete, ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar
MBUNGE wa Jimbo la Kojani, pia ni Naibu Wazairi wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hamad Hassan Chande, akicheza ngoma ya msewe na wakati kikundi cha ngoma hiyo kilipokua kikitoa burudani, wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kiwanda cha kusarifia Mwani Chamanangwe Wilaya ya Wete, ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar.

 

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)