Na Maryam Talib – Pemba.
HAKIKA kuweza nikujiwezesha hakuna kitu kinachokuja bila ya kujishuhulisha hayo ni maneno ya bwana Hamad Salim mwenye umri wa miaka (65) alipoamua kuanzisha shamba lake la viungo lililopo sehemu moja inayopatikana Gando katika shehia ya Gando mkoa wa kaskazini Pemba.
Kilimo cha viungo ni fursa adhimu iliyopuuzwa na kufichika katika Kisiwa cha Pemba ambayo kama ingetumiwa vyema na wakaazi wa kisiwa hichi ingekuwa na manufaa makubwa hasa hasa kwa utalii wa ndani na kwa wananchi wa kawaida .
Hata hivyo kuna fursa moja muhimu iliyofichika kwa wakaazi wa kisiwa cha Pemba ambayo takribani miaka saba sasa anaitumia Bwana Hamad Salim wa Gando nayo ni ya kilimo cha viungo ikiwamo kilimo cha vanilla, hiliki, midalasini, tangawizi, majano, pilipili manga na viungo venginevyo.
Hamad alisema “mtaka cha mvunguni hadi ainame” lakini pia ukitaka kuiga uige kilicho na faida kama alivofanya yeye mpaka kufikia hatua ya kumiliki shamba lake la viungo ambalo kwa sasa amekuwa akitembelewa mpaka na watalii wa ndani jambo ambalo alisema kwake anahisi ni faraja kubwa ambayo inaweza kumletea tija kwa haraka sana ambapo wazo hilo la kuanzisha shamba hilo lilimjia baada ya kuona soko la vanilla lilivo kubwa kwa kuona kuwa kilo ya vanilla ni shilingi milioni moja japo kuwa yeye hajafikia kiwango hicho ila taratibu ndio mwendo.
Bwana hamadi kwa sasa alisema ameshaanza kuvuna vanilla na kuuza kilo saba Pamoja na pilipili manga kilo thelethini ikiwa kilo moja ya vanilla ni shilingi laki nne za kitanzania na pilipili manga shilingi elfu ishirini kwa kilo jambo ambalo limeshaanza kumpatia faida kubwa ikiwemo kujenga nyumba ya tofali ya kuishi na Watoto Pamoja na kusomesha Watoto wake kwa pato la shamba hilo la viungo.
Alisema hakuna kitu kinachokuwa kizuri kama hakijashuhulikiwa kwa kina kama serikali imeamua kuboresha utalii katika kisiwa cha Pemba ikiwamo utalii wa viungo basi yeye amepiga hatua moja nyengine anaiyomba serikali kutia nguvu katika shamba lake la viungo kwa kuongezewa huduma ikiwamo kupelekewa mashine ya kupelekea maji kwani hiyo mimea chakula chake kikuuu ni maji na kujengewa vyoo na maboresho mengine ambayo yanaweza kulikuza Zaidi shamba hilo ili liwe la utalii kama Mh.Rais wa Zanzibar alivoadhimiria kukuza utalii katika kisiwa cha Pemba.
Hata hivyo amesema hakujikita kwenye shamba la viungo tu kwani “haba na haba hujaza kibaba”kwa kujiongeza kwa kufuga nyuki ambapo aliesema kwa sasa asali imekuwa na soko kubwa pia amekuwa akiuuza hapo hapo akiwa na mizinga thelethini kwa sasa ambapo amekuwa akiuza asali kwa lita elfu ishirini na tano hivyo ameiomba serikali walitambue shamba lake na kuliboresha ili liwe la kiutalii rasmi.
Sada Hamadi Salim mwenye umri w amia (31) ambae ni mtoto wa Bwana hamad nae ni mmoja anaeshirikiana na baba yake katika kulikuza shamba hilo la viungo ambapo alisema unapopata upetee kata kama wanavofanya wao kwa kulienzi shamba la baba yao na kulishuhulikia ipasavyo mana wamekuwa wakinufaika nalo sana kwa kuwawezesha matumizi mbalimbali nyumbani na maslahi mengine muhimu ni kuiyona serikali tu sasa kwamba inasimama na wao katika kuliboresha kulifanya kuwa la kitalii katika kisiwa cha Pemba.
Kwa upande wake Mdhamini Wizara ya Utalii na mambo ya kale Zuhura Mgeni alisema kwa kuipongeza jumuiya waandishi wa Habari kisiwani Pemba (Pemba Press Club) kwa kuunda mbinu ya kutembelea vivutio vya utalii kisiwani Pemba kwani alisema mwenye “kulishwa haachi kushiba” nguvu ya Pamoja inazaa vitu vingi kila mmoja kwa chombo chake akihabarisha umma juu ya suala zima la vivutio vya utalii Pemba tunaweza kupata mafanikio ya haraka katika kisiwa chetu cha Pemba.
Utalii ni suala mtambuka ambapo kwa sasa hata wananchi wa kisiwa cha Pemba wameshaujua thamani yeke na yote haya yamekuja baada ya kupatiwa mafunzo elekezi ya mara kwa mara kupitia wizara husika yanayohusiana na utalii kusudi kuondokana na dhana potofu kwenye eneo hilo lakini hata hivyo tija imeaanza kuonekana sasa kwani wengi wao wanaufurahia utalii katika maeneo yao hususan Mkoa wa Kaskazini Pemba ambako ndiko kuliko na vivutio vingi vya utalii.
Mdhamini huyo alisema ukioneshwa njia mzuri ifuate kwani Mh Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi aliposema yuko tayari kukifungua kisiwa cha Pemba kiutali na lazima Pemba ifungunke hivyo na wao Wizara ya Utalii wanaunga mkono jududi hizo katika kuitangaza na kutoa elimu kama ambavo wanajua kwamba sekta ya utalii ni sekta mtambuka na ndio inayoingiza pato la nchi ikiwa ni asilimia 30 hivyo jumuiya ya waandishi wa habari Pemba imefanya jambo zuri la kuandaa ziara hiyo ya kutembelea vivutio hivyo vya utali kwa kutoa muangaza kwa kuelimisha jamii kwa kupitia vyombo vya Habari kisiwani hapa.
“Mcheza kwao hutunzwa”ni maneno ya Zuhura Ofisa Mdhamin Wizara ya Utalii kama Wizara wao wanasema mtunza Mh, Rais ni kusimamia zile juhudi zake kama alivoamua kuikuza Pemba kiutalii kwa kuvitunza na kuvilida na kuvitanganza vivutio hivo vya utaliiili kuleta haiba na kubaki na haibayake ambayo ipo kwa kufanya usafi wa mara kwa mara na kupanda miti ili kuondosha uporomoko ya hali ya uharibifu wa mazingira.
Zuhura alisema kwa upande wa kisiwa cha Pemba kwenye suala la utalii limekuwa hususan wananchi wa kisiwa cha Pemba hasahasa wananchi Mkoa wa Kskazini Pemba wameelimika na kuufurahia sana suala utalii kwani wanajua kuwa suala la utali ni suala mtambuka sasa suala hilo ni jukumu lao kuhakikisha utalii unasimama na pia utalii unaimarika katika kisiwa hichi katika kuisaidia nchi yetu katika kupata mapato kupitia sekte hii.
Akifafanua kwa upande wa Pemba vivutio vya utalii kisiwani hapo vipo vingi ikiwamo Chwaka Tumbe,Pango la Watoro, Pango la Kijiji Makangale, ,Shamba la viungo Gando, Shamba la viungo Mtambwe,Rasi Kiuyu pia na Vumawimbi vyote hivyo ni vivutio vya utalii kisiwani Pemba katika Mkoa wa Kaskazini na pia Mkamandume kwa upande wa Mkoa wa Kusini Pemba.
kwa upande wake Mwenyeti wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba Bakar Mussa Juma alisema lengo kuu la waandishi wa jumuiya hiyo kufanya ziara hiyo kway a kuyatembelea maeneo ye vivutio vya utalii kisiwa Pemba ni kwa lengo la kuyatangaza mambo mbali mbali yanayofanya kwenye utalii na katika sekta tofauti kuyasemea yaliyofanya katika serikali ya awamu ya nane na kuunga mkono juhudi za Mh, dk. Mwinyi ya kukiinua Kisiwa cha Pemba.
UTALII KISIWANI PEMBA UNAWEZEKANA.
MWISHO.