Monday, January 27

Usawa wa kijinsia unahitajika katika shuhuli za uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

AFISA Ufuatiliaji na Tathmini katika mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili Doroth Nyoni

NA ABDI SULEIMAN.

AFISA Ufuatiliaji na Tathmini katika mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili Doroth Nyoni, amesema katika utekelezaji wa mradi huo wamezingatia fursa sawa kwa makundi yote, ikiwemo suala la elimu  ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

Alisema katika ufuatiliaji na tathmini ambao wamefanya wameona ushirikishwaji wa makundi yote wakiwemo wanawake, vijana, Watoto na walemavu, inasababisha rasilimali zote zinzopatikana kwenye hifadhi kuwa salama, kwa kila mwana jamii ni mnufaika.

Alisema tayari wanawake 756 kati ya 1872 wameshafikiwa na mafunzo ikiwemo katika ngazi za juu za vijiji, ili kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye shuhuli za uhifadhi.

Akiwasilisha mada ya usawa wa kijinsia na uhifadhi, hivi karibuni kwa wana chama cha waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET) kuhusu umuhimu wa kuzingatia jinsia kwenye masuala ya uhifadhi na Mazingira.

“Huu mradi malango yake ni kuwajengea uwezo wanawake 1872, kwenye eneo la uongozi na mpaka kufikia sasa zaidi ya wanawake 756 wameshafikiwa,”alisema.

Nyoni alisema Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, unatekelezwa katika shoroba saba ikiwemo Kwakuchinja, Amani Nilo, Udzungwa na Hifadhi ya Nyerere, Ruaha Rungwa na Katavi, Ruaha Rungwa na Inyonga na Kigosi Moyowosi Burigi Chato, ambapo umezingatia usawa wa kijinsia kwa kuwezesha makundi yote kushiriki katika shughuli za kiuchumi.

Alisema mazingira na shuhuli za uhifadhi zinapoharibika wanawake ndio wahanga wakubwa wakupata shida, kutokana na kukosekana kwa mahitaji muhimu na kulazimika kufuata masafa marefu, hali inayopelekea kukumbwa na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.

Aidha alisema tayari mabadiliko yameanza kujitokeza kwa wanawake baada ya kupata elimu ya uhifadhi wa shoroba, wapo wanaongoza wenzao na wengine kushiriki katika suala la ulinzi baadhi yao wamejiunga katika vikundi vya uhifadhi.

Akizungumzia suala la vijana, Doroth alisema kupitia kampeni mbali mbali zimefika katika skuli, ili kuwafundisha watoto juu ya kuhifadhi mazingira na maliasili zake kwenye maeneo wanayoishi kulingana na uwelewa wao.

Alisema elimu mbali mbali imeshatolewa na sehemu kubwa elimu hiyo imetolewa kwenye korido ya kwakuchinja na Amani Nilo ambako mafanikio yake yameanza kuonekana.

Mwenyekiti wa JET Dr.Ellen Otaru, alisema uanzishwaji wa vikoba na ujasiriamali wa aina mbali mbali kama utengenezaji wa vitu kwa ajili ya watalii, ufugaji wa nyuki, kwani dunia sasa inapigania suala zima la usawa wa kijinsia.

Alisema mwanamke ni mzalishaji mkubwa kwenye familia, kwani wanawake ndio wanaohusika zaidi katika kilimo kuliko wanaume na watumiaji wa mfumo wa uzalishaji kwenye ardhi, ikiwemo chakula, kuni, mkaa na vitu vyengine.

“Sio mtumiaji wa kulisha familia lakini hata uzalidhaji wa mali ghafi zinapatikana kwenye ardhi, ndio maana tunasena mwanamke lazima ashirikishwe kwenye masuala yote ya kuboresha adrhi na utunzaji wa mazingira,”alisema.

Hata hivyo aliwataka wanawake kushirikishwa katika sera, sharia na mambo yanayoendelea katika jamii, kwani yatasaidia sana kumfanya mwanamke kutokuingia katika makossa ambayo yasioyakwake.

Nae mwandishi wa habari Rahma Suleiman, alisema mazingira yanapoathirika hayamuachi nyuma mwanamke, mtoto na mwanamme wote wanakua ni wahanga, hivyo ni vizuri kushirikisha wanawake katika suala zima la uhifadhi.

Alisema wanawaake wamekua wakiathiriwa na matukio ya ujangili wanayofanya waume zao, kwa kutokujua shuhuli wanazozifanya waume ambazo sio halali.

MWISHO 

Abdi Juma Suleiman

Journalist/Photographer

Zanzibarleo newspaper/habari Portal.blog
Chake Chake -Pemba
+255774565947 or +255718968355