Monday, September 16

MAONYESHO YANATOA FURSA KWA WANAFUNZI-WAZIRI LELA

NA ABDI SULEIMAN.

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Lela Mohamed Mussa, ameipongeza Wizara yake kwa kuratibu ufanyikaji wamaonyesho ya elimu ya juu Unguja na Pemba kwa miaka mitano sasa, ikiwemo kitengo cha elimu ya juu.

Alisema kuwepo kwa maonyesho hayo ni kutoa fursa kwa wanafunzi kupata usajili na taarifa za ukweli na uhakika kwa wanafunzi, jambo ambalo wazazi walikua wakilipia ada katika vyuo ambavyo havijasaliwa.

Waziri lela aliyaeleza hayo alipokua akizungunza na wanafunzi wazazi na watendaji kutoka wizara ya elimu, akifungua maonyesho ya elimu ya juu Kisiwani Pemba.

Alisema kuwepo kwa maonesho hayo yamesaidia wazazi na wanafunzi kujua uhakika wa nini wanachokwenda kukosoma na vyuo vya kwenda kusoma kwa usahihi.

“Wanafunzi sasa wanajua chuo kipi kimesajiliwa na chuo kipi tunachokwenda kujiunga nacho, pamoja na fursa mbali mbali za udahili na mikopo kwa kujiendeleza elimu ya juu,”alisema.

Alisema ufaulu unaongezeka vyuo vinapata nafasi ya kupata wateja wao wa kujiunga na vyuo hivyo kupitia usajili kwa wanafunzi waoakwenda kuomba kujiunga.

Hata hivyo alisema maonyesho hayo yanatoa fursa kwa vyuo kupata wanafunzi wanaotaka Zanzibar, kwani wanafunzi wengi wanaenda kujiunga na vyuo hivyo kutokana na huduma bora wanazozitoa.

Waziri lela alisema vipo vyuo vinatoa ithibati kwa taasisi zinazotaka kuanzisha vyuo hivyo, alizipongeza taasisi zote zilizoshiriki katika maonyesho hayo.

Hata hivyo alizipongeza taasisi zote zilizoamua kushiri katika maonesho hayo, kwa kutoa huduma hata ndani ya kisiwa cha Pemba, lengo ni kuwaondoshea usumbufu wananchi wa kisiwa cha Pemba.

Katika hatua nyengine waziri lela, alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wabaraza la Mpainduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa hatua kubwa ya maendeleo aliopiga ndani ya kisiwa cha Pemba.

Akizungumzia suala la Amani alisema, Amani haipatikani kwa mtutu bali inapatikana kwa maendeleo ndio jambo ambalo viongozi wa SMT na SMZ wanaendelea kulifanya hivi sasa.

Nae Naibu katibu Mkuu utawala wizara ya elimu na mafunzo ya amali Khalid massoud Waziri, alisema maonyesho hayo yanawasaidia wanafunzi waliomaliza elimu zao za sekondari kupata mambo mbali mbali, ikiwemo kusaidiwa ujazaji wa fomu bila malipo.

Alisema pia wanafunzi wanapata kusajiliwa na taasisi mbali mbali za mikopo ya elimu ya juu, kwa ajili ya kupata mikopo mbali mbali ya kujiunga na vyuo vikuu pamoja na mabenk ya kifedha.

“Maonyesho haya ni muhimu sana kwa wanafunzi waliomaliza elimu yao ya kidato cha sita, kupata fursa mbali mbali za kujiunga na vyuo,”alisema.

Aidha naibu huyo waziri alisema maonyesho hayao kawaida hupangwa kila matokeo ya mitihani ya kidato cha sita yanapotolewa, muda ambao vijana hao wanapata muda wa kwenda kuomba vyuo mbali mbali vya ndani nan je ya nchi.

Alisema mwaka 2024 wanafunzi wengi wamafanikiwa kwa kiasi kikubwa, na wanafunzi hao karibu wote wanasifa za kujiunga na vyuo vikuu.

Hata hivyo naibu huyo alimuhakikisha waziri wa elimu kuwa maonyesho hayo yanamanufaa makubwa kwa maendeleo ya vijana katika elimu ya juu na wataendelea kuyatayarisha kila mwaka na kuyaendeleza.

Nao baadhi ya vyuo vilivyoshiri katika maoneshi hayo ya elimu ya Juu Pemba, wamesema maonyesho hayo ni muhimu kwao kwani wanafunzi wanapata kujiunga moja kwa moja na vyuo bila ya malipo.

Walisema wanafunzi wengi wameitikia wito wa kufika na kupata uwelewa juu ya vyuo na taasisi za mikopo za Tanania bara na ile ya Zanzibar.

Nao wanafunzi waliomaliza masomo yao kidato cha sita, wameishukuru Wizara ya Elimu Zanzibar kwa kuwaandalia maonesho yao, kwani wanaweza kusajiliwa na kuungwa na vyo mbali mbali nadani na nje ya nchi.

MWISHO