Sunday, November 24

MKUU WA WILAYA CHAKE CHAKE AWAPOKEA VIJANA 12 KUTOKA KOREA

WANAMICHEZO 12, walimu na viongozi wa Taasisi ya KFHI wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba na kupokelewa na wanafamilia zao, mara baada ya kuwasili Kisiwani Pemba baada ya kuibuka mshindi wapili katika nchi 10 kwenye mashindano ya Hop Cup yaliofanyika nchini Korea.(PICHA NA ABDI SULEIMAN)

NA ABDI SULEIMAN.

MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, amesema serikali ya Wilaya na Mkoa wa Kusini Pemba imefarajika sana, na uwakilishi mkubwa uliofanywa na vijana katika mashindano ya Hop Cup nchini Korea.

Alisema ushiriki wao mzuri katika mataifa 10 umewafanya kurudi na mshindi wa pili katika mashindano ya kombe la Matumaini, kwani kutoka Wilaya ya Chake Chake.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya mapokezi ya vijana hao, huko katika uwanja wa ndege wa Pemba alisema ushiriki wao na ushindi walioupata ni jambo la faraja na kutia moyo katika mashindano.

“Mutakumbuka kuwa siku hile mulioondoka niliwambia kama nyinyi ndio waakilishi pekee kwa Tanzania, munakwenda kuiwakilisha nchi licha ya kutoka kwenu Kisiwani Pemba, hilo mumelitekeleza na mshindi wa pili mumerudi nao,”alisema.

Alisema serikali ya Wilaya imefurahi kwani muweza kwenda kuutangaza utamaduni, vipaji na hata utalii na lugha yetu ya Kiswahili ambayo wageni wengi wanatamani kujifunza.

Hata hivyo aliwashukuru waandaaji wa mashindano hayo, kupitia KFHI kwa kuwapeleka katika maeneo mbali mbali ikiwemo vyuo vikuu na maeneo ya kujifunnzia.

MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, akiwaongaza wazazi katika kuwapokea wanamichezo 12, walimu na viongozi wa Taasisi ya KFHI, katika uwanja wa ndenge wa Pemba, mara baada ya kuibuka mshindi wapili katika nchi 10 kwenye mashindano ya Hop Cup yaliofanyika nchini Korea.(PICHA NA ABDI SULEIMAN)

Nae Mwalimu wa wanafunzi hao Sadiki Bakar, aliwashukuru wazazi kwa kuwaruh  usu watoto wao kwenda nchini korea kushiriki mashindano hayo na kurudi salama, kwani lengo ni kwenda kushindana kupitia mchezo Hop Cup.

Aidha aliyataja baadhi ya mataifa mengine waliokwenda kushindana nao ni pamoja na Nchi ya Bokinafaso, Zambia, South Africa, Tanzinia, Gontanama, Sirilanka, Korea na Vetnam.

Hata hivyo alisema safari yao hiyo pia waliweza kuutangaza utalii wa Tanzania, hususana Zanzibar katika maeneo mbali mbali ambayo walikua wakitembelea.

Akizungumzia suala la utamaduni, alisema wamefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika suala la zima la utamaduni, kwa kushindana na mataifa zaidi ya 10.

MWISHO