Monday, January 27

VIKWAZO WANAVYOPITIA WAGOMBEA WANAWAKE WANAPOINGIA KWENYE UONGOZI.

 

NA – AMINA AHMED

Pemba: “Sikuwa na fedha,maeneo mengine sikuweza kuyafikia ,Elimu ya uongozi sina Chama kilikosa ya kuniwezesha kifedha  na safari yangu kwa mwaka 2020 ikaishia asante kwa kushiriki  jambo ambalo halikuwa kusudio langu’’ Amesema Riziki Mgeni.

Wahenga waliosema kuwa ‘’Mkono Mtupu Haurambwi‘’ Wakiwa na maana ya kuwa unapofanyiwa jambo lolote hata kama unahitaji usaidizi basi ni lazima uwe na kitu  kidogo cha kuongezea ambacho  sio ahsante ya mdomo mtupu,wakaendelea kusema kuwa ‘’Mti Hawendi Bila ya Nyenzo’’ yaani ni lazima upate wasaidizi katika kufika safari yako uliokusudia .

Ndivyo hivyo ambavyo imetokea kwa Riziki Mgeni Juma mzaliwa wa Wilaya Chakechake  yenye jumla ya wakaazi  25,201  Wadi ya Vitongoji yenye wakazi  6394  (wanaume)  3,050 na  3,344 (wanawake) ambaye anaamini mkononi wake ungekuwa na kitu angeweza kuviepuka vikwazo vya kisiasa  na kuwa mmoja kati ya Diwani wa kuchagulia  na wananchi Wadi ya Mtambwe mwaka  2020  na kuwa  mtetezi wa changamoto za jamii yake hiyo.

Riziki  mwenye umri wa miaka 42,Mkaazi wa Wadi ya Mtambwe yenye wakaazi  16,237 ( wanaume) 80 13 (wanawake) 8,224 mama wa 6  ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Chadema -BAWACHA  Mkoa wa Kaskazini Pemba  ambapo kwa sasa mwanamke huyo  ni Mwenyekiti wa Barza hilo Kanda ya Pemba.‘’ Wanawake tunajitokeza na tuna mwamko sana wa kujitokeza kugombea nafasi za uongozi lakini kuna vikwazo vinavyotukwaza sisi wanawake  kwanza ni uwezeshwaji  hatufikii malengo ya kuwa viongozi kwa sababu ya uwezeshwaji  na kukosa fedha’’.  Amesema Riziki huku akiongeza kuwa ‘’Uwezeshwaji wa kifedha binafsi nilishindwa kuzifikia sehemu zote kunadi sera zangu nikaishia kushika nafasi ya tatu ,naamini maeneo ambayo sikuyafikia ningeliyafikia basi saivi ningelikuwa diwani nawatumikia wana Mtambwe lakini sikuwa na uwezo  na sehemu nyengine zilihitaji gharama’’Amemaliza Riziki.

Zanzibar  yenye jumla wanawake 974,281   sawa na asilimia  51.6 na  wanaume 915,492 sawa  48.4  sensa ya watu na makaazi  ya waka 2022 kati ya hao ni asilimia (21.14) sawa na wanawake 71    waliojitokeza kuwania nafasi za udiwani  ambapo Chama cha Demockrasia na Maendeleo CHADEMA kilisimamisha wagombea kwa asiliamia 7 kwenye  nafasi hiyo.

Ikumbukwe kuwa  Tume ya Uchaguzi Zanzibar-ZEC kupitia Sera ya ushiriki wa kijinsia  2015 pamoja na mambo mengine imekuwa na dhamira njema ya  kuwahamasisha  wanawake  kushiriki  katika uchaguzi  kama wapiga kura na wapigiwa kura .‘’Chama changu kilikosa rasilimali fedha kipindi kilichopita na ikapelelea kukosa zile fedha za kufanyia kampeni kwa hiyo tuliwezeshwa tu kielimu mule mule ndani ya chama sisi wagombea ila sio kwa upana wake ambayo ingekuwa yenye kutusaidia ingawa sio kwa ukubwa” Amesema Rziki.

Amesema ‘’Pia tulitakiwa tushindane kwa sera,hoja , bila kujali itikadi zetu za kisiasa tulitakiwa tujengewe uwezo wa kujitambua kuwa sisi ni kitu kimoja  tena ibakie wananchi wenyewe tu tena kuchagua wanawake kwa mujibu wa Sera zetu’’ Amesema Riziki

Omar Nassor ni Mwenyekiti wa Chama cha  Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA amesema kuwa “Chama chetu kimekuwa kikiwasaidia wanawake kutimiza malengo yao ikiwemo  kugombea nafasi za uongozi  ambapo kuanzia nafasi za  ndani ya chama ,sambamba na  zile za majimboni jambo ambalo limefanikiwa na kuweza ushiriki wa  wagombea wanawake katika  nafasi nyingi   za majimbo kuanzia udiwani uwakilishi na ubunge walijitokeza’’ Amesema Omar wakati akizungumza na Mwandishi wa Makala hii.

Aisha Abdalla Juma ni Mwanaharakati maswala ya wanawake wenye ulemavu  kutoka shirikisho la Jumuiya za watu wenye ulemavu  Zanzibar SHIJUWAZA amesema kuwa ipo  haja kwa serikali kutoa ruzuku maalum kwa ajili ya wagombea wanawake ambayo itawasaidia kuzikabili changamoto hizo.

”Bila kubagua  itikadi  wala udogo wa vyama  serikali ituangalie kwa upekee sisi wanawake hususan ni wale ambao wnakuwa wakijitolea kuwania nafasi mbali mbali iwawezeshe ruzuku kwa kutambua kuwa kundi hili kwa muda mrefu tumeachwa nyuma katika ushirikishwaji’’  Alisema Aisha Abdalla  .

‘’ Ulazima huo  wa kuwapata viongozi wanawake unahitaji kupaziwa sauti maalum ambazo zitasaidia kuishawishi Serikali kuweka ulazima wa kisheria hata kwa vyama vidogo ambazo zitasaidia kuwawezesha  katika uchaguzi na harakati zake.” Muhammed Suleiman mkaazi Madungu.

Riziki anaiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,wadau wa maendeleo kwa wanawake ikiwemo Chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA ZNZ kuendelea kutoa elimu kwa wagombea wanawake sambamba na kuwasapoti  ili waendelee kushiriki katika harakati hizo  za kutafuta nafasi za uongozi “Kuwaezesha kitaaluma , kifedha pamoja na usalama wao bila kujali tofauti za siasa wala udogo wa vyama vyao  walivyo  huku akiamini kuwa uwezo na umakini walio nao viongozi wanawake wanapo  kuwa viongozi , ni ukombozi wa changamoto za  jamii  zao “ Amemaliza Riziki.

MWISHO