Monday, January 27

MCHANGO WA WAANDISHI NA VYOMBO VYA HABARI KWA VIONGOZI WANAWAKE.

FATMA Juma  Khamis  Diwani  wa  Tibirinzi  Chake chake   yenye jumla ya wakazi 11,089 wanawake ) 5,785  (wanaume)  5,304  ambaye  anawachukulia waandishi wa habari  na vyombo vya habari kwake kama ndugu zake wa damu  .

Hii ni kutokana na yeye kufanya kazi  kwa ukaribu zaidi na wanahabari kabla ya kuzianza harakati hizi za siasa na uongozi mnamo mwaka  2000.

Fatma Juma Khamis mwenye umri wa maiaka 42 Mzaliwa na mkaazi wa  Msingini Chake  Chake  Mkoa wa Kusini Pemba mtaa wenye  idadi ya wakazi 2,748 (wanaume ) 1,286 (wanawake) 1,462  na kaya 517 ,Mke na mama wa watoto 4, mwenye elimu ya kidato cha 4 ambae licha ya nafasi hiyo ni mtaalamu katika masuala ya utoaji wa huduma za kijamii ikiwemo ushauri masuala ya afya  na mazinagira.

 

Haumuwii  vigumu kuvitumia vyombo vya Habari na waandishi   katika kuonesha uwezo na uwajibikaji wake katika nafasi aliyo nayo sasa ya udiwani.

‘’Napenda  vyombo vya habari na nathamini mchango wake kwangu,na navitumia sana vinanitangaza , sitosahau siku ambayo nilipaza sauti changamaoto  ya barabara,na vyoo na kupata wahisani wa kurekebishwa na kutengenezwa  kwa nafasi yangu   vilipata ufumbuzi Jambo ambalo najivunia kila siku .

‘’Kabla kujiingiza katika siasa mimi nilikuwa nafanya kazi shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kama mhudumu mengi nilijifunza , mafanikio waliyokuwa wanayapata wananchi  kupitia  wanahabari, wanapata msaada , pongezi kwa uwajibikaji  yote hayo hayakuja bure kama sio kulitumia daraja hili katika kufika safari zao.

‘’Kulinijengea uzoefu wa kujiamini,ujasiri na kujitangaza jambo ambalo limeifanya  akili yangu kuona umuhimu wa tasnia hii katika kutimiza malengo niliyonayo ambapo  kwa sasa nikifanya jambo lolote kwa nafasi yangu siwaachi ni msaada mkubwa kwangu.” Amesema Fatma.

Anaamini kuwa wapo viongozi anaowazidi katika kuwatumia wanahabari licha ya udogo wa nafasi yake ukilinganisha nafasi za juu za viongozi wengine ambao wamekosa uthubutu wa kutumia vyombo vya habari,jambo ambalo anatamani liwe mfano wa kuigwa na watu wengine kutoka kwake.

‘’Kuna viongozi  wenzangu wakike na wakiume wanakosa kuvitumia vyombo vya habari ,wapo wanavichukulia easy na wapo wanaogopa kuvitumia tu licha ya nafasi walizo nazo wanaishia  kutokujulikana licha ya nafasi zao’’

Mkoa wa kusini Pemba wenye jumla ya wilaya mbili Chake Chake na Mkoani  umebarikiwa kuwa na Jumla ya madiwani 35  19 kati ya hao ni kutoka wilaya ya Chake chake ambapo wanaume  07 na 12 wakiwa ni  wanawake  huku Wilaya ya mkoani nayo ikiwa na idadi ya madiwani 16 na mlingano sawa wa jinisia katika baraza hilo la madiwani.

 

Hali ipo tofauti kidogo kwa Diwani wa kuchaguliwa  na Wananchi  wadi ya Matale iliyopo nje kidogo na Mji wa Chake chake Time Ramadhan Khatib (45) mama wa Watoto 8 ambae licha ya nafasi hiyo  ni mzoefu katika  maswala ya huduma za afya jamii  ,aliyeanza harakati zake  za kupenda siasa tangia akiwa skuli  ya sekondari mwaka 1994 na kushiriki mikutano  ya Chama ,  anawalaumu waandishi wa Habari wakike kisiwani Pemba kwa kuendelea  kujifungia ndani bila kujua ni wapi wanapatikana wanapohitajika.

‘’Vyombo vya habari na waandishi wa habari wananisaidia sana ila bado kuna shida  ya kujifungia ndani waandishi wanawake  hatuwaoni kabisa  na wala hatujui tunawapata wapi kwa hapa kwetu Pemba’’.

‘’ Natumia mwandishi mmoja mwanaume   ambae  kazi zangu naziona na napokea pongezi  ,wengine   sijui nawapata wapi wanajifungia sana huyu alinitafuta  na wao wajitoe kututafuta wanawake wenye uthubutu tupo wengi hususan ni huku vijijini’’.

Zanzibar ambayo ina kisiwa kuwa na idadi ya waandishi wa Habari 350 ,kati ya hao 176 (wanawake) huku 174 (wanaume) ,Vyombo vya habari 90  na waandishi wapatao 100 wakiwa ni wanachama wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tamwa Zanzibar ambapo   licha ya idadi hiyo bado wahitimu kutoka vyuo vikuu na vya kati wanaendelea kuhitimu  na  kwa mujibu wa  Kamisheni ya vyuo vikuu Tanzania -TCU jumla ya wahitimu  800,000 katika fani tofauti ikiwemo habari kuhitimu na kuhitaji ajira sawa na idadi ya wahitimu milioni moja kwa mwaka.

”Tunashangaa ni kwasababu gani viongozi wanawake hawafanyi kazi  sana na vyombo vya Habari haijawahi kutokea kumuona kiongozi mwanamke kaitisha mkutano na waandishi wa habari kama wanavyofanya wenzao wanaume  huku kwetu jambo ambalo tunajiuliza wana changamoto gani na vyombo vya habari na fursa zipo‘’ Said Omar Said  Meneja wa Mkoni fm amesema.

‘’Hata kuwatumia waandishi wanawake katika kazi zao pia ni gumu na ni wachache wanafanya hivyo, labda ni utayari wa hao viongozi au wanakwepa usumbufu wa kujitoa” Amemaliza.

Bakar Mussa Juma yeye ni mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Pemba PPC yenye idadi ya waandishi wa habari wapatao 61 wanaume 26 wanawake 35 amesema kuwa mchango wa waandishi kwa viongozi wanawake umekuwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma hii ni kutokana na walio wengi kujikita katika kuwaandikia wanawake ,licha ya kuwa hawawatumii kwa kiasi kikubwa katika Habari zao kama vyanzo vikuu vya taarifa.

”Nashindwa kuwatumia viongozi wanawake katika habari zangu sababu nakosa mashirikiano baadhi yao hawana utayari mtu unaweza ukamfuta akawa anakupiga danadana mpaka unaona ni bora uachane nae ufanye kazi nyengine na mtu mwengine hata bila kuzingatia jinisia” Amesema Thureya Ghalib Mwandishi wa Habari Pemba.

’’Wapo wengi ambao tunawatumia katika Habari zetu na wanatutafuta kila wanapokuwa na kazi sijui ni sababu gani zinawafanya wengine washindwe kutuamini na kututumia sisi wanawake wenzao katika kujitangaza ila wanaotaka kututumia tunakuwa nao bega kwa bega wapo wawakilishi masheha wabunge pia’’.Amesema

Juhudi hizi za kuandika habari zinazohusu maendeleo kwa wanawake kupitia vyombo mbali mbali pia ni miongoni mwa mchango wa Chama Cha waandishi wa habari wanawake Zanzibar Tamwa  ambao kwa Asilimia kubwa wamekuwa wakiongeza hamasa kwa wanahabari na vyombo vya habari kuandika habari za viongozi wanawake,ambapo kuputia juhudi hizo za  kutetea ili kuweza kuufikia  Usawa wa Kijinsia katika nyanja mbali mbali ikiwemo Uchumi Siasa na Demcrasia.

Ambapo juhudi hizo  umedhihirika na  kwa Mujibu  TamwaZanzibar  jumla ya stori  2101 kutoka mwaka 2020 /2023  zimezalishwa na waandishi wa vyombo mbali mbali vya Habari ikiwemo  Makala za Gazeti,Makala za mtandaoni na vipindi vya Redio.

MWISHO