Sunday, November 24

Wazazi wanaowafuatilia watoto wao kwa njia ya simu

.

Elain Spector alikuwa na wasi wasi wa kutaka kuskia iwapo mtoto wake wa kiume alikuwa amerejea salama kwenye bweni lake huko Texas, baada ya kuwatembelea nyumbani hivi majuzi.

Lakini badala ya kusibiri apige simu au atume ujumbe, mama huyo kutoka Baltimore nchini Marekani, aliendelea na shughuli zake za siku akisubiri ujumbe kutoka kwa simu yake.

Hii ni kwa sababu sawa na watu wengine milioni 32 kote duniani, Spector na familia yake yote wameweka app ya Life360 kwenye simu zao.

App hiyo inafuatilia walipo kila mara watoto wake watatu, na kumjulisha wakati wako safarini, wanapofika salama nyumbani, kama wako mahali hawastali wawe na data zingie.

Wakifika shuleni inalia, wakifika nyumbani inalia, anasema Spector, ni njia ya sisi kujua kama famialia mahala kila mtu alipo.

Wameitumia app hiyo kwa miaka kadhaa sasa, na Spector anasema licha ya watoto wake wana tbia ya kuzimo sehemu walipo wakati mwingine, mtoto wake mkubwa wa kiume amekuwa na utulivu wa kuitumia.

Licha kuwa kwa sasa ana umri wa miak 18 na anaishia mbali nao, anakiri kwa yeye kutoa app hiyo inamuacha na mkazo wa mawazo.

App za kufuatilia familia, zimepata umaarufu wa haraka kwa muongo mmoja uliopita na zaidi. Hitaji la kulinda watoto wake ni sehemu ya kukua lakini app zinazdifi kuongezeka wakati wazazi wengi wanaendelea kuhisi kuwa dunia inazidi kuwa eneo hatari.

Wataalamu wanasem wazazi walio na nia kuzitumia app hizo ni lazima wafikirie jinsi watazitumia na vile watazungumza na watoto wao kuzihusu. App hizi zinaendelea kuboreka zaidi na pia aina ya data zinazokusanya na kuibua maswali kuhusu usalama wa mtu binfasi.

Na watoto ambao wamelewa wakifuatiliwa kwa njia za app sasa wanafikia utu uzima na kuwaachia wazazi na maswali – kuhusu ni lini watazima app hizo?

Geofencing, ufuatiliaji wa kasi na mengine mengi

App ya Life360 inatumiwa sana na famialia nyingi – kwa sasa iko nafasi ya sita kati app zinazopakuliwa sana katika ghAla la app za iOS nchini Uingereza na Marekaji – bado kuna app zingine kadhaa zote zinazowapa wazazi viwango tofauti vya kuwafuatilia watoto wao.

Ghislaine Bombusa, mkuu wa kampuni ya Internet Matters ya nchini Uingereza, inawashauri wazazi kuhusu usalama wa mitandao anasema kuna aina mbili ya ufuatiliaji. Kuchagua kati ya hizo inahusu aina ya malezi yako na ni kwa ukaribu gani ungependa kumfuatilia mtoto wako.

Zilizo rahisi zaidi ni app za kutambua maeneo zinazokujazikiwa tayari zimewekwa kwa simu kama zile za Find My Friends kwenye vifaa vya iOS au Google Family kwa vifaa vya Android. Pia kuna app zinazo wawezesha watumiajia kukusanya data kutoka simu zingine.

Hii ni pamoja na teknolojia kama ile ya geofencing ambapo ujumbe hutumwa wakati simu inangia au inatoka eneo fulani. Kwa hivo wazazi ambao watoto wao ni madereva, kuna teknolojia ya kufuatilia kasi na ya kutambua ajali kitu ambacho Spector anasena amekipata kuwa cha umuhimu mkubwa.

Credit: Life360)

Huduma zinazotolewa na Life360 ni nyingi

CHANZO CHA PICHA,LIFE360)

Kwa teknolojia iliyoboreka zaidi ya app kama FindMyKids humruhusu mzazi kuwasha akiwa mbali kinasa sauti kweye simu ya mtoto na hata kurekodi huku teknolojia ya TeenSafe inajigamba kuwa tekelnolojia inatofanya mzozo asiweze kujua iwapo mzazi wake anamfuatilia.

Kando la kufuatilia, app zinaweza kuongoza maisha ya kidijitali ya mtoto ikiwa ni pamoja na jinsi wanavyotumia pesa, na ni michezo ipi wanashiriki, anasema Bombusa. Apps kama OurPact zinaruhusu mzazi kuona picha za sikrini za mawasiliano ya mtoto mitandaoni huku app ya Bark huwa inapiga ujumbe picha na kumtumia mzazi.

App hizi ni biashara kubwa. Life360 pekee inakadiriwa kuwa ya thamani ya dola bilioni 1 ikiwa inatumiwa kwenye zaidi ya nchi 140.

Data dhidi ya uaminifu

App zinazotumiwa kufuatilia hujiuza kama vifaa muhimu kwa wazazi kwenye dunia inayokumbwa na hatari. Zinategemea wazazi ambao wataamini kuwa iwapo wanajua mahala watoto wao wapo, watakuwa salama au watoto wengene watajizuia na tabia hatari ikiwa watajua kuwa wafuatiliwa.

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Na kumekuwa na visa ambapo wazazi wametumia app hizo kuwapata vijana ambao wamepata ajali au hata wametekwa.

Lakini Sonia Livingstone, profesa katika idara ya habari na mawasiliano katika chuo cha London School of Economics anaamini kuwa hakuna ushahidi kuwa app hizi huwaweka watoto salama.

Watengezaji wa app na wale wanaofanya matangazo ya biashara wanalenga kuwafanya wazazi kuamini kuwa kuapata app ni kitendo cha kuonyesha mapenzi watoto lakini kitu muhimu zaidi kwa maendelea ni kuwa mtoto anajifunza kumuamini mzazi na mzazi hivyo hivyo kwa mtoto, anasema Livingstone.

Lakini vijana wengine na hata wake walio na umri mkubwa wanahisi kuwa wazazi wao wanaingilia haki zao.

Kwenye ujumbe mmoja ulochapishwa katika mtandao wa Reddit ulisema: “Mama yangu alikuwa ameona kuwa nilikuwa nimezima eneo nilikuwa katika app ya Life360 na kunitishia kuzima simu yangu na pia akaniambia kuwa siwezi kuendesha gari tena…Oh pia nilitaja kuwa nina umri wa miaka 20???

Livingstone anasema kuna hatati kuwa kuwafuatilia watoto inaweza kugeuka kutoka kuwaingilia hadi kuwadhulumu .

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Wataalamu wanasema ni bora kuzungumza na watoto kuhusu kuibadilisha programu hiyo wakati wanapoendelea kuwa wakubwa

Mipaka na usawa

Iwapo mzazi anahisi kuwa app ndiyo njia bora kwao, pia lazima wajue kumpunguza hatari ambazo zimezungumziwa na Livingstone.

Bombusa anasema ni muhimu kuwa matumizi ya app ni kitu ambacho wazazi na watoto wanastahili kufanya kwa pamoja baada ya mjadala ulio wazi.

Hakikisha kuwa kila upande unaelewa kile teknolojia hiyo inaweza kufanya, kwa nini unaihitaji, ni mipaka gani unaweka na cha muhimu mtomo anahisi vipi kwa hilo. Anaongeza.

Ni mihimu pia kuelewa kuwa vile mtoto anaendela kukua anahitaji uhuru zaidi.

“Nafikiri ni kuhusu tabia mtoto wako anaonyesha. Kama waliitumia mara ya kwanza walipopata simu na kufuata sheria….kuna uwezekanoakwa mjadala kuhusu kuachana na baadhi ya vifaa vya kufuatilia. Au pia kusema kuwa ni sawa nitafuatilia wakati nitahisi kuwa kuna hitaji la kufanya hivyo badala ya kila wakati.”

Spector anajivuna kuwa familia yake ina mjadala wazi unaoependwkezwa na Bombusa kwa hivyo hafuatilii sana watoto wake.Lakini anakiri kuwa sio rahisi kuachana na ujumbe unaotumwa na app ya Life360 na utulivu wa akili anaoupata anapoona mahala walipo watoto wake.