


NA ABDI SULEIMAN.
ZAIDI ya wananchi 127 wamepiama afya zao, pamoja na kuchanja chanjo ya COVID 19 katika bonanza maalumu la Afya kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani Kisiwani Pemba.
Aidha wananchi 67 waliweza kupima afya zao juu ya HIV na wananchi 60 waliweza kupata chanjo ya JJ, SPUTINIK LIGHT na SINOVAC, pamoja na upimaji wa Presha.
Bonaza hilo lililofanyika katika uwanja wa michezo Gombani na kushirikisha michezo mbali mbali, ikiambatana na upimaji wa afya za wananchi katika maradhi mbali mbali yanayowasumbua.
Akizungumza na Vijana na wananchi mara baada ya kupokea maandamano yaliyoanzia Machomanne hadi Gombani, Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba, Salum Ubwa Nassor, aliwataka vijana kuhakikisha wanaendelea kulinda afya zao ili kujikinga na maradhi mbali mbali ikiwemo nyemelezi.
Alisema vijana wanapopima na kujuwa afya zao, nirahisi kujitambua na kuendelea kuilinda dhidi ya vishawishi mbali mbali vilivyowazunguruka.
“Panapotokea mabonanza kama haya ni vizuri vijana kujitokeza tukapima afya zetu, ili tuweze kujijua tuko katika hali ngani, hivi sasa maradhi ni mengi sana na mengine huwezi kuyaona mapaka ukapime”alisema.
Aidha alisema kufanyika kwa mabonanza kama hayo yanatoa fursa kubwa kwa vijana na wananchi, kwenda kupima afya zao tafauti na siku nyengine kwenda katika vituo vya afya.
Naye Mkurugenzi Msaidia ZAC Sihaba Saadat, alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2016/2017 Tanzania nzima, unatathmini maambukizi ya ukimwi iko vipi kwa Tanzania ikiwemo Zanzibar na kuonyesha kuwa Zanzibar ina 0.4% ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.
Alisema utafiti huo uliangalia uwelewa wa jamii na watu wazima, umeonyesha vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 ni 25% tu wenye uwelewa sahihi juu ya Ugonjwa wa Ukimwi.
Aliwataka vijana kuhakikisha wanalinda afya zao na kutambua tahamani yao katika nchi, kwani vijana ndio tegemeo la taifa la kesho.
Kwa upande wao wananchi waliohudhuriwa bananza hilo, aliishukuru Tume ya Ukimwi kwa kuweka bonanza hilo na kupima afya zao, kwani vijana inakua ngumu kwenda katika vituo vya afya kuma.
MWISHO