Thursday, October 31

VIDEO: Wakufunzi wa mradi wa kuza kilimo Zanzibar wapatiwa elimu.

NA MCHANGA HAROUB-PEMBA.

Wakufunzi wa mradi wa kuza kilimo zanzibar wametakiwa  kuwa tayari na kujitolea kwa  kuwafika wakulima katika maeneo mbali mbali  ili elimu ya kilimo biashara iweze kuwafikia walio wengi na kuleta matokeo yaliokusudiwa.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh, Mattar Zahor Masoud wakati akifunga mafunzo ya awamu ya pili ya wakufunzi hao huko katika ukumbi wa Green Foliage Chake Chake Pemba.

Amesema Serikali imekusudia kutoa pesa nyingi kwa wajasiriamali na wakulima wadogo wadogo lakini bado kuna tatizo la utaalamu, hivyo kujitolea kwao kufundisha kwa ari kutasaidia serikali kuwa na wazalishaji wengi wenye utaalamu.

Akisoma risala ya wakufunzi hao Habiba Issa Mohamed amesema mafunzo hayo ni muhimu kwao kwani yatawawezesha kuendeleza kilimo chenye tija ambacho kitasaidia kukuza uchumi wa vijana na taifa kwa ujumla.

Mkuufunzi mkuu wa mafunzo hayo kutoka taasisi ya AHA (Bibla Pichila) amesema mafunzo hayo yanalengo la kuwasaidia vijana kuendeleza kilimo biashara ili waweze kupata tija juu ya wanachozalisha.

Mradi wa kuza kilimo Zanzibar unaendeshwa na taasisi ya TRIAS, AHA na  TAHA na kufadhiwa na umoja wa nchi za ulaya  (European  union) ,  lengo lake kubwa ni kuwajengea uwezo wakulima wadogo wadogo na wajasiriamali wa zanzibar, kimuarisha lishe pamoja  na kujiwekea mtaji.

KUANGALIA VIDEO HII BOFYA HAPO CHINI.