Monday, November 25

Habari Picha, Kijana Hai Foundation yazindua mradi wa Miliki Uwezo .

MKURUGENZI Mtendaji wa Kijana Hai Foundation Erick Godfrey Ramsey, akitoa maelezo juu ya mradi wa Miliki Uwezo unaotekelezwa na Kijana Hai Foundation, juu ya uwezeshaji wanawake kiuchumi kukuza usawa wa kijinsia,kuondoa umaskini na kuendeleza Uchumi Shirikishi, hafla iliyofanyika Mjini Chake Chake
MKALIMANI wa Lugha za Alama Pemba Asha akitoa maelezo kwa kutumia ishara ya alama, wanawake wenye ulemavu wa kutokusema wakati wa Uzinduzi wa mradi wa Miliki Uwezo unaotekelezwa na Kijana Hai Foundation.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Miliki Uwezo unaotekelezwa na Kijana Hai Foundation, hafla iliyofanyika mjini Chake Chake
BALOZI wa Canada nchini Tanzania Pamela O’donnell akizungumza na wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wakati wa uzinduzi wa mradi wa Miliki Uwezo unaotekelezwa na Taasisi ya Kijana Hai Foundation, halfa iliyofanyika mjini Chake Chake
BAADHI ya washiriki wa halfa ya uzinduzi wa Mradi wa Miliki Uwezo, unaotekelezwa na taasisi ya Kijana Hai Foundation, hafla ya uzinduzi imefanyika Mjini Cghake Chake

 

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)