Wednesday, October 30

VIDEO: DC Mkoani alishukuruku shirika la UNESCO kwa kuiunga mkono Wilaya hio.

NA  KHADIJA KOMBO-PEMBA

Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja amelishukuru shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni  (UNESCO) kwa juhudi zake za kuiunga mkono Wilaya hio kwa miradi mbali mbali ya maendeleo ndani ya jamii.

Mkuu huyo wa Wilaya ametoa pongezi hizo huko ofisini kwake wakati alipokutana na Mkurugenzi Mkaazi na Mwakilishi wa  UNESCO nchini Tanzania aliyefika Ofisini kwake huko Mkoani mara baada ya uzinduzi wa kituo cha Makuzi na malezi ya watoto huko Skuli ya Msingi Mkanyageni katika Wilaya ya Mkoani.

Amesema Serikali ya Wilaya inathamini juhudi za Shirika hilo na kuahidi kufanya kazi nao kwa pamoja ili kuinua ustawi wa jamii hasa watoto katika upatikanaji wa elimu.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkaazi na mwakilishi wa  UNESCO nchini Tanzania Bwana Tirso dos Santos  Amesema kwa kufahamu umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike wamekuwa wakiweka mazingira mazuri ya kujisomea ili kupunguza wimbi la utoro maskulini.

Mapema akizindua Kituo  cha makuzi na malezi huko Skuli ya Msingi Mkanyageni Mkurugenzi huyo amewataka wanajamii kutoa mashirikiano ya kutosha katika kukitunza na kukiendeleza kituo hicho ili kiweze kuwa endelevu kwa manufaa ya watoto wote.

Kituo hicho cha Makuzi na malezi kimejengwa kwa ufadhili wa UNESCO kwa kushirikiana na Jamhuri ya watu wa  Korea.

KUANGALIA VIDEO HII BOFYA HAPO CHINI.