NA ABDI SULEIMAN,
MUFTI Mkuu wa Zanzibar Shekh Saleh Omar Kaabi, amewataka wananchi wa sompiya kuwa na moyo wa kushirikiana, katika kutatua matatizo ya jamii zao na maeneo ya jirani, ili amani na utulivuo iendelea kudumua.
Mfufti Mkuu aliyaeleza hayo wakati alipokua akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu na wananchi wa shehi ya Sompiya, mara baada ya kufungua mskiti kijijini hapo.
Shekh Kaabi alisema pahala patakatifu katika ardhi ni mskitini, kwani mskiti usipotumiwa kwa kusali utawasuta, hivyo unapaswa kutumiwa kufanya ibada na kuwahimiza watoto kusali.
“Tunapaswa kuutumia msiki kwa mambo mema, ikiwemo kuweka darsa mbali mbali, kuwasomesha watoto wetu mambo mema, tutumie pia kusuluhishana migogoro inayotoka katika jamii”alisema.
Naye katibu wa Muft Shekh Khalid Ali Mfaume, alisema hivi sasa miskiti ni sehemu ya wailamu kujuwana, kuelimishana, sehemu ya kutunza amani, kusaidia mayatima, wajane na kuwaelimisha vijana juu ya athari za matumizi ya madawa ya kulevya, ubakaji, udhalilishaji.
Akitoa nasaha juu ya umuhimu wa mskiti sheikh Khamis Salum Ali, alisema jukumu kubwa la mskiti ni kuwakutanisha waumini, kushikamana na kuwa kitu kimoja na kuepukana na migogoro isiyo ya lazima.
Aidha aliwasihi waumini kuhakikisha wanayaendeleza yale yote yalioachwa na Mtume (S.A.W), kwani nifaraja kubwa kwa waumini na wananchi wa Sompia.
“Sote ni mashahidi siku hizi kumekua na misikiti mingi inajengwa, kujengwa kwake tunapaswa kuitumia ipasavyo katika kufanya ibada, tumekua tukishuhudia migogoro mingi inatokea pale mskiti unapokua na vitenga uchumi, basi imani za waumini zinaanza kuchafuka”alisema.
Akisoma risala ya wanajamii wa Mkungu Malofa, ustadhi Salum Hamad alisema mskiti huo unatarajiwa na waumini waliopo katika kijiji cha Smpia na ameneo ya jirani ikiwemo kijiji cha Minazini.
Aidha alisema msikiti huo unakadiriwa kuchukuwa waumini wasiopungua 200 kwa wakati mmoja,huku wakiamini kuwepo kwa msikiti huo itakuwa ni chachu ya kuzidisha idaba na matumizi bora ya watoto, akinamama na wanajamii kwa ujumla kwani wanahitaji kuwa na madrasa kwa ajili yao.
MWISHO