Wednesday, October 30

IDARA ya Katiba na msaada wa Kisheria wawafikia wananchi kisiwa cha Fundo

 

MKURUGENZI wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria kutoka Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Hanifa Ramadhan Said, akifungua mkutono wa kutoa elimu kwa jamii katika siku 16 za kupinga masuala masuala ya udhalilishaji wa jinsia, kwa wananchi wanaishi katika kisiwa cha Fundo Wilaya ya Wete.(
WASANII wa Sanaa ya Maigizo kutoka Wete Awena Hamad Khamis (kushoto) na Hudhaifat Ali Amour (kulia), akimpatia kanga mama yake amsomee jina lililoandikwa, akionyesha athari za kutokujua kusoma kwa mtoto wakike, wakati wa utoaji wa elimu kwa jamii katika siku 16 za kupinga masuala masuala ya udhalilishaji wa jinsia, kwa wananchi wanaishi katika kisiwa cha Fundo Wilaya ya Wete.
BAADHI ya wananchi wa Kisiwa cha Fundo Wilaya ya Wete, wakifuatilia kwa makini mkutano wa utoaji wa elimu kwa jamii katika siku 16 za kupinga masuala masuala ya udhalilishaji wa jinsia, kwa wananchi wanaishi katika kisiwa cha Fundo Wilaya ya Wete, mkutano ulioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria zanzibar
AFISA Sheria kutoka Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar Yusra Abdalla Said, akitoa maelezo kwa wananchi wa Kisiwa cha Fundo juu ya Changamoto mbali mbali za udhalilishaji wanazokumbana nazo katika jamii, wakati wa utoaji wa elimu kwa jamii katika siku 16 za kupinga masuala masuala ya udhalilishaji wa jinsia, mkutano ulioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria zanzibar

NA ABDI SULEIMAN.

WANANCHI Kisiwa cha Fundo Wilaya ya Wete Kisiwani Pemba, wamesema ipo haja sasa kupitiwa upya kwa sheria NO:6 ya 2018 ya Makosa ya Jinai kifungu Namba 108, ili iweze kuwatia hatiani wahusika wote wawili wa matendo hayo(Mwanamke na Mwanamme) na sio kama ilivyo sasa.

Wananchi hao wamesema matendo hayo ya udhalilishaji na ubakaji wa wanawake na watoto, hayatoweza kupungua iwapo sheria hiyo kama itaendelea kumtia hatiani mtuhumiwa wa kiume Pekee na kumuwacha wa kike.

Wakitoa maoni yao katika mkutano wa kutoa elimu kwa jamii, katika siku 16 za kupinga masuala masuala ya udhalilishaji wa jinsia, kwa wananchi wanaishi katika kisiwa cha Fundo Wilaya ya Wete, mkutano ulioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar.

Mwajuma Rashid Saleh kutoka kijiji cha Ndooni Kisiwani Fundo, alisema ipo haja kwa serikali na wadau kuibadilisha sheria ya Ubakaji, ili iweze kutoa hukumu kwa watu wote kwa lengo la kukomesha matendo hayo.

“Sheria hii munayoijuwa nyinyi imebezi Upande mmoja, wakati wafanyaji wa tendo ni watu wawili kwanini na mwanamke nae asihukumiwe kama ailivyo mwanamme”alisema.

Alisema ikiwa hukumu ya ubakaji na udhalilishaji anapatiwa mmtu moja tu, matendo hayo yataendelea kutokea mpaka mwisho wa duniani, na itafika wakati wanawake watakuwa wengi mitaani na wamaume wengi magerezani kutokana na kuhukumiwa wao tu.

Naye Abdalla Salim Ali mkaazi wa Fundo, alisema wakati umefika kufanyia au kupitia upya kwa sheria ya Makosa ya jinai kifungu namba 108 ili kumtia hatiani na mwanamke kama ilivyo kwa manamme.

Alisema wanawake ndio wanaoficha siri za majumbani mpaka zinapowashinda ndipo wanapowashirikisha wwenza wao, kwa hatua zaidi za ufumbuzi kutokana na kuwakingia vifua watoto wao.

Aidha aliwataka akinamama kuacha kuwashonea au kuwaruhusu watoto wao wa kike, kuvaa nguo za kubana na kutoa majumbani nguo ambazo zinapelekea matamanio kwa wanaume.

Akifungua mkutano huo Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria kutoka Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Hanifa Ramadhan Said, alisema lengo la mkutano huo ni kuelimisha jamii juu ya kupinga masuala yote ya ukatili na udhalilishaji, licha ya masuala ya ukatili kutokumgusa mwanamke pekeyake bali hata wanaume.

Alisema jukumu la malezi ni la wanafamilia na sio mwanamke pekee, kama inavyofikiriwa hivi sasa huku akiwataka wananchi kutoa changamoto zao ikiwemo masuala ya ardhi, ndoa, ili kupatia ufafanuzi wa kisheria.

“Sisi kama idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria, tumelazimika tufike Fundo baada ya kuona wenzetu wa WEPO hawawezi kufika Visiwani na elimu ikawa inahitajika”alisema.

Akitoa ufafanuzi wa maswali ya wananchi, Wakili wa Serikali Juma Mussa Omar, aliwataka vijana kutokushawishika na mavazi ya wanawake na kupelekea kuharibu mila na tamaduni zao.

Huku akiwasihi wazazi kujitahidi kuwavisha watoto wao wakike mavazi ya heshima na sio kuwapatia nguo zinazowabana, ambazo zitapelekea kuwavunjia heshima na kupelekea vishawishi kwa jamii.

MWISHO