Wednesday, October 30

VIDEO: Samaki aleta maafa Wilaya ya Micheweni.

NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.

Watu watatu wamefariki dunia na wengine 28 kulazwa katika Hospitali ya Micheweni kutokana na kula chakula aina ya samaki anaedaiwa kuwa na sumu .

Akizungumzia kuhusu tukio hilo  Daktari  wa Wilaya ya Micheweni Dr, Mkubwa Habib amesema tayari watu hao ambao wamefika katika hospitali hio wakitokea Msuka wanaendelea kupatiwa matibabu , lakini changamoto kubwa waliyoipata ni kukosa mashirikiano mazuri kutoka kwa wahanga hao jambo ambalo liliwawiya vigumu kuwapatia tib asahihina kwa haraka.

Kwa  Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Micheweni  Bi Mgeni Khatib Yahya amesema hadi hivi sasa hajapata idadi kamili ya watu ambao wamekula samaki huyo, hivyo amewataka wananchi wote ambao wametumia chakula hicho kufika Hospitali ili kuchunguzwa zaidi afya zao.

Kwa upande wake mmoja kati ya wazazi waliofikwa na maafa hayo amesema.

Tukio kama hili liliwahi kutokea katika miaka ya 90  huko katika shehia  ya Vitongoji na watu wasiopungua 20  walifariki dunia.

KUANGALI VIDEO HII BOFYA HAPO CHINI