NA ABDI SULEIMAN.
LICHA kupata msaada wa kujengewa Matundu 12 ya Vyoo na Mdau wa Maendeleo, lakini bado matundu hayo hayajakidhi mahitaji ya wanafunzi wa skuli ya Ole Msingi Wilaya ya Chake Chake katika suala la vyoo.
Skuli hiyo yenye wanafunzi 1849, inahitaji angalau matundu ya vyoo 50, ambalo tundu moja litaweza kutumiwa na wanafunzi 37 kwa wakati mmoja.
Matundu hayo yameweza kujengwa na mdau huyo, kufuatia taarifa iliyoatolewa na Gazeti la Zanzibar leo Toleo NO:6335 la Septemba 8/2021 ukurasa wa tano inayosema skuli ya kosa vyoo wanafunzi wajisaidia vichakani, msiktini na toleo NO:6425 Novemba 16/2021 ukurasa wa 12 na 13 inayosema Uhaba wa vyoo waikabili skuli ya ole Msingi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, kufuatia ujenzi huo wa matundu 12 ya vyoo Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Ole Msingi Ali Mussa Ali, alisema licha ya matundu hayo 12 kuwepo lakini bado hayajakidhi mahitaji ya wanafunzi wa skuli hiyo.
“Skuli inawanafunzi 1849 na walimu 36, tuna matundu 12 itakuwa tundu moja kwa wanafunzi wasiopungua 168 na walimu 36 wamepata tundu moja, vitaweza kutusaidia japo kidogo tafauti na tulivyokua hatuna hata tundu mmoja”alisema.
Alisema mahitaji halisi ya vyoo ni kuwa na matundu yasiopungua 50 ambapo tundu moja litaweza kutumiwa na wanafunzi 36 hadi 37 kwa wakati mmoja, hivyo vyoo vilivyopo vitaweza kupunguza tataizo la wanafunzi kwenda kujisaidia vichakani, miskitini na majumbani kwa sasa.
Aidha aliwataka wadau kujitokeza kusaidia, kwani bado wanahitaji vyoo zaidi ndi, ili kuondosha kilio chao cha muda mrefu, vyoo vina umuhimu mkubwa na ndio sehemu muhimu ya mahitaji ya binaadamu, kwani vyoo vinapunguza maradhi mbali mbali ya mripuko katika sehemu za majumbani.
“Ila lile tataizo limeweza kupungua na tunaringia kuwepo kwa matundu 12 ya vyoo vya kisasa, japo kuwa ile changamoto haijaondoka mara moja ila imepungua kidogo”alisema.
Naye Mwalimu wa skuli hiyo Said Salum Hemed, alisema hali ilikua ngumu sana na walishindwa kuwadhibiti watoto katika suala zima la kujisaidia, kwani watoto wengine ni wakubwa kama darasa la tano na sita.
Mwalimu wa jinsia skuli ya Ole Saada Hamad Mbarouk, alisema vyoo vilivyopo vitaweza kuwasaidia wanafunzi wao kujihifadhi, ikizingatiwa wanafunzi wengine ni wakubwa ikiwemo wanafunzi wakike na wakubwa.
Alisema vyoo hivyo licha ya kuwa ni kidogo ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi, lakini vimefika wakati muwafaka kutokana na dunia sasa kukubwa na matendo ya udhalilishaji wa wanawake na watoto na ubakaji.
Kwa upande wake afisa uwendeshaji tiba Pemba kutoka Wizara ya Afya Ustawi wa jamii wazee na Jinsi na Watoto, Dr.Yussuf Hamad Iddi, kwa mujibu wa W.H.O tundu moja la vyoo linapaswa kutumiwa na wanafunzi 15 walioko bodingi na wanafuzi 25 kwa sio kaa bodingi.
“Kitaalamu hiyo ndio inavyotakiwa katika mahitaji ya vyoo, lakini inategemea na idadi ya wanafunzi kwa skuli, ila tunapojenga skuli tunapaswa kuzingatia na mahitaji ya vyoo”alisema.
Akizungumzia umuhimu wa vyoo, alisema ni kupunguza maambukizi ya maradhi mbali mbali, huki wakiwakata walimu kuhakikisha wanadumisha usafi mara kwa mara ili kupungza madhara kwa wanafunzi.
Naye Rais wa Skuli ya Ole Msingi Amina Ali Hassan, alimshukuru mdau huyo wa maendeleo, kwa juhudi na uwamuzi wake kuwapatia vyoo kwa ajili ya kuwanusuru wanafunzi na vitendo vya udhalilishaji kama wangeendelea kujisaidia vichakani.
Alisema tatizo la ukosefu wa vyoo lilikua likiwaumiza vichwa kila wakati, kwani muda mwengine walikuwa wakikosa masomo kutokana na kuutumia wakiwa majumbani kujisaidia.
Mariyamu Othaman Yahaya Mkaazi wa Ole, aliwaomba wadau wa maendeleo na serikali, kuangalia sehemu iliyobakia ya vyoo na kuweza kuvimaliza, ili wanafunzi wapate sehemu sahihi na kwa idadi maalumu ya wanaotumia vyoo na kuepukana na maradhi.