Monday, November 25

VIDEO: Jumla ya wananchi 120 kutoka katika shehiya saba za Jimbo la Chambani wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali.

NA KHADIJA KOMBO- PEMBA.

 

Wakaazi wa Jimbo la Chambani katika Wilaya ya Mkoani wameushukuru Uongozi wa Jimbo hilo kwa juhudi zao za kuwapatia mafunzo ya ujasiri amali ambayo yata wakomboa katika kuinua hali zao kiuchumi.

Wakizungumza baada ya mafunzo hayo huko katika shehiya ya ukutini Washiriki hao wamesema mafunzo hayo yameweza kuwapatia ujuzi ambao watautumia katika maisha yao na kuimarika kiuchumi

Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo Fasad Salanga kutoka Dar es Salaam amewataka washiriki hao kuyatumia vyema mafunzo hayo huku wakiongeza ubunifu ili waweze kupata manufaa zaidi ya kimaendeleo katika kuinua jimbo lao.

Naye Mwenyekiti wa Madi katika Wilaya ya Mkoani Mohammed Said amesema Kitendo cha Viongozi wao kuleta mafunzo hayo kumesaidia Serikali katika kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa Vijana katika jimbo hilo.

Wakipokea pongezi hizo Mwakilishi wa Jimbo Hilo Mh. Bahati Khamis Kombo na Mbunge MH. Mohammed Abdulrahman Mwinyi wamesema wameamua kuleta mafunzo ya ujasiriamali kwa wananchi waJ imbo hilo ili kuhakikisha wanainua maisha ya wananchi waJimbo la Chambani hivyo wamewataka wananchi hao kuyatumikia vyema mafunzo hayo kwa malengo yaliyokusudiwa.

Jumla ya wananchi mia moja na ishirini (120) kutoka katika shehiya saba za Jimbo hilo wamepatiwa mafunzo hayo ikiwa ni Pamoja na utengenezaji wa Batiki, Usindikaji wa Pilipili, Utengenezaji wa Jiki Pamoja na sabuni.

 

 

KUANGALIA VIDEO YA MAFUNZO HAYO BOFYA HAPO CHINI