NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.
Katika kuelekea Maadhimisho ya siku kumi na sita (16) zakupinga ukatili wa kijinsia Umoja wa Vilabu vya mazoezi Kisiwani Pemba kwa Kushirikiana na Jumuiya ya Waandishi wa Habari wanawake Tanzania kwa Upande wa Zanzibar ( TAMWA ZANZIBAR) pamoja na Jumuiya ya watu wenye ulemavu wa Akili ( ZPDD) wameandaa Bonanza maalum ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mapambano dhidi ya Vitendo vya Udhalilishaji kwa wanawake na watoto
Akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo tofauti vilivyoko Kisiwani Pemba Mkurugenzi wa TAMWA Zanaibar DR Mzuri Issa amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kupambana na Vitendo vya Udhalilishaji wa kijinsia hivyo hakuna budi kila mmoja kwa nafasi yake kuunga mkono juhudi hizo.
Kwa Upande wake Katibu wa Vilabu vya Mazoezi Pemba Khalfan Amour Mohammed amesema wameamua kushirikia na na taasisi hizo katika kufanikisha bonanza hilo kwani vilabu hivyo vinanafasi kubwa ya kushiriki katika mapambano hayo.
Bonanza hilo ambalo linatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 11/12/2021 wakati wa saa 12 asubuhi litatanguliwa na matembezi maalum ambayo yataanzia madungu hadi Gombani na kuongozwa na Wakuu wa Mikoa yote miwili ya Kisiwani Pemba.
KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI