Sunday, November 24

WANAFUNZI wa Vyuo vikuu vilivyopo Kisiwani Pemba watoa ya moyoni.

NA ABDI SULEIMAN.

WANAFUNZI wa Vyuo vikuu vilivyopo Kisiwani Pemba, wamewashauri wanafunzi wenzao kusimama kidete kupiga vita vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na watoto nchini.

Wamesema hilo linawezekana kufanyika ipowa watakua kitu kimoja kwa vyuo vyote, kutoa elimu kwa jamii hususana vijijini juu ya kupiga vita vitendo hivyo vinavyoathiri maisha ya wanawake na watoto.

Waliyaeleza hayo mjini chake chake, wakati wa kongamano la siku 16 za kupiga vita vitendo vya udhalilishaji na ubakaji wa watoto, lililoambatana na utoaji wa elimu ya Haki za Binaadamu na udhalilishaji.

Manur Juma Khamis kutoka chuo cha Mwalimu nyerere, aliwataka wanafunzi wenzake kuhakikisha elimu hiyo wanaifikisha katika maeneo yao wanayoishi ili kuona mabadiliko ya jamii.

Salim Seif Sai kutoka IPA, alisema wakati umefika kwa shehria ya makosa ya jinai kufanyiwa mabadiliko, ili kuweza kuwatia hatiani wahusika wote wawili wa matendo ya udhalilishaji na sio mwanamme peke yake.

“Matendo haya yanapofanyika lazima mwanamke na mwanamme anahusika, vizuri kama mwanamme miaka 15 basi na mwanamke miaka 10 au saba na nusu, hapo tutaweza kuyapunguza kutokea na kusikika”alisema.

Azra Assa Hamad kutoka IPA, alisshauri ZLSC kuendelea kutoa elimu mbali mbali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, kwani muda mwingi wanakuwa na jamii na wanaweza kuifika selimu hiyo kwa wakati muwafaka.

Kwa upande wake Hadia Khamis, alisema ulevi ni moja ya chanzo kinachopelekea kutokea kwa vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na watoto nchini.

Naye Mwanasheria wa Kituo cha Huduma za sheria Zanzibar Tawi la Pemba Siti Habibu Mohamed, alisema nijukumu la kila mtu kupiga vita vitendo vya udhalilishaji, ili kuweza kupata taifa lililokuwa bora na lenye maadili mema.

Afisa mipango wa ZLSC Safia Saleh Sultani, alisema malamalimiko yamekua mengi juu ya sheria ya udhalilishaji, huku wananchi wakitaka kufanyiwa mabadiliko ili kuwatia hatiani wahusika wote wawili.

“Wanafunzi munapaswa kuzisoma na kuzijua kikamilifu sheria mbali mbali zilizopo nchini, kwani kutokujuwa sheria sio sababu ya kuzifunja na adhabu zake ni kali sana”alisema.

Mapame akifungua kongamano hilo la vyuo vikuu, katika siku 16 za kupiga udhalilishaji Afisa Mdhamini Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala la Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalumu za SMZ Thabiti Abdalla Othman, alisema suala la udhalilishaji limekua linakera kila mtu, hali iliyofanya serikali ya awamu ya nane kuimarisha mifumo ili kutaka kuliondosha katika jamii.

Hata hivyo aliwataka wananchi kutokuwafumbia macho watendaji wa matendo hayo, na kuhakikisha wanawafikisha katika vyombo vyua sheria ili hatua kuchukua mkondo wake.