Sunday, November 24

PPC wakutana na wadau wa Amani Kisiwani Pemba.

WADAU wa Habari kutoka taasisi mbali mbali ikiwemo Viongozi wa Dini, vyama vya siasa na asasi za kiraia, wakifuatilia ufunguzi wa Kongamano la kuhamasiha Amani ya Kweli, lililoandaliwa na Klabu ya waandishi wa habari Pemba (PPC) kupitia mradi wa SAUTI YANGU, AMANI YANGU, HATMA YANGU, kongamano lililofanyika mjini Chake Chake
MWENYEKITI wa Klabu ya Waandishi wa Habari Pemba (PPC)Bakari Mussa Juma, akifungua Kongamano la Kuhamasisha Amani ya Kweli kwa wadau habari Pemba wakiwemo Viongozi wa Dini, Vyama vya Siasa na Asasi za Kiraia, kupitia kupitia mradi wa SAUTI YANGU, AMANI YANGU, HATMA YANGU, kongamano lililofanyika mjini Chake Chake
Dk.Ali Yussuf Ali, akiwasilisha mada juu ya dhana ya amani katika kongamano la kuhamasisha Amani ya Kweli, kongamano lililowashirikisha Viongozi wa Dini, Vyama vya Siasa na Asasi za Kiraia, kupitia kupitia mradi wa SAUTI YANGU, AMANI YANGU, HATMA YANGU, kongamano lililofanyika mjini Chake Chake

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

NA ABDI SULEIMAN.

KLABU ya waandishi wa habari Kisiwani PEMBA (PPC)imesema inakusudia kuendeleza historia ya kuwepo kwa amani ya kudumu katika kisiwa cha Pemba kama ilivyokuwa zamani kwa kuelimisha jamii kujuwa wajibu wao hasa wakati wa harakati za uchuguzi.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa PPC Bakari Mussa Juma, wakati akifungua kongamano la kuhamasisha amani ya kweli lililowashirikisha Viongozi wa Dini, vyama vya siasa na asasi za kiraia, ikiwa ni Utekelezaji wa Mradi wa SAUTI YANGU, AMANI YANGU, HATMA YANGU, kongamano lililofanyika mjini Chake Chake.

Alisema Kisiwa cha Pemba kinasifiwa sana kwa kuwa na amani ya kweli na ukarimu katika nchi mbali mbali duniani, hivyo ni vyema kushirikiana katika kuirejesha historia hiyo kwa jamii kujenga utamaduni wa amani ya ndani ya nafsi zao.

“Hilo linathibitika kufuatia viongozi wa taasisi ya Friends of Zanzibar, walipokuaja Pemba wamesema “Pemba ni moja ya sehemu pekee yenye amani na utulivu, kuliko nchi mbali mbali ambazo wamepita Pemba nambari moja kwa kuendeleza Amani”alisema.

Aidha aliwataka wadau hao kutumia nafasi zao katika kushajihisha jamii, vijana, wanawake na watoto kuendelea kudumisha amani iliyopo kwani ndio tunu pekee ya Zanzibar na kisiwa cha Pemba.

Mwenyekiti huyo alisema maendeleo yoyote ya nchi hayawezi kufikiwa iwapo hakutakua na amani, hivyo bado Zanzibar inaendelea kuwa sehemu salama kwa wananchi wake na kupiga hatua kimaendeleo kutokana na uwepo wa amani ya kwenli.

Hata hivyo aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanakuwa karibu na vijana wao, ili kutokuwaazima akili zao wanasiasa katika wa uchaguzi na kutokuingia katika vurugu.

Akiwasilisha mada juu ya dhana ya amani katika kongamano hilo, Dk.Ali Yussuf Ali, alisema amani iliyopo ni tunu ya visiwa vya Zanzibar, hivyo ni lazima jamii ione umuhimu wa kuwepo kwa amani hiyo kwa maslahi ya jamii na taifa.

“Kutokana na umuhimu wa amani hakuna dini yoyote inayopiga vita wala kuhimiza vurugu, bali dini zote zinahimiza amani, umoja na mshikamano, huku akiwataka wananchi kuwa mstari wambele katika utunzaji.

Wakichangia katika kongamano hilo, wadau hao wamesema wakati umefika kwa wananchi kurudi katika kitabu cha kur-an, ambacho wamekisahau ili kuweza kupata dawa ya suluhisho la uvunjifu wa amani.

Fatama Ali Khalid, alisema suala la ulevi linachangia kwa akiasi kikubwa uvunjifu wa amani Nchini, kwani mtu anapolewa lolote anaweza kulifanya.

Naye Hasima Hamad Khamis, alisema suala la udhalilishaji kama halitokomeshwa basi litapelekea uvunjifu wa amani, kwani wananchi wamekosa amani pale watoto wao wanapokwenda skuli au vyuo vya kuruani.

Kwa upande wake Salum Khamis Juma, aliishauri PPC kuendelea kutoa elimu ya Utunzaji wa amani kwa wananchi wote, huku wakijikita zaidi vijijini kwani ndiko ambako elimu hiyo imekosekana.

Innati Aboubakar aliwashauri vijana kujiunga katika vikundi vya ushirika, ili kunufaika na fedha za Dr.Mwinyi na kupelekea kutokukubali kushawishiwa kwani watakua na kazi za kufanya.

Mradi huo wa miezi sita unaotekelezwa na PPC wakishirikiana na Foundation for civil society na Search for common Ground, kwa ufadhili wa umoja wa nchi za ulaya.