NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.
Masheha Kisiwani Pemba wametakiwa kuhakikisha wanajaza taarifa sahihi za kaya zilizomo ndani ya shehiya zao katika daftari la shehiya ili kusaidia Serikali kupanga mipango ya maendeleo ya wananchi wake kwa usahihi.
Wito huo umetolewa na Afisa Mdhamini Tume ya Mipango Pemba Maalim Khamis Issa Mohammed alipokuwa akizungumza na masheha hao kwa nyakati tofauti huko katika Ofisi za Wilaya zao ikiwa ni katika hatua ya kuhamasiha ujazaji wa taarifa katika daftari la shehiya kwa maendeleo ya nchi.
AmesemaTume ya mipango Serikalini ndio inayopanga mipango yote ya maendeleo ikiwa ya muda mrefu na mfupi hivyo taarifa hizo ndio zinazowezesha kupanga mipango hio kwa ufanisi.
Kwa upande wao Maafisa Mipango Tume ya Mipango Omar Makame Juma na Mwadini Haji Kheri wamesema katika kufuatilia ujazaji wa madaftari hayo wamegundua kuwa kuna matatizo mengi yanayojitokeza ikiwa ni uwelewa mdogo kwa wajazaji wa taarifa hizol akini pia bado jamii haitowi mashirikiano ya kutosha katika kutekeleza kazi hio.
Hivyo wamewataka wananchi kufahamu umuhimu wa daftari hilo kwani endapo litajazwa vizuri na kwa usahihi litaweza kusaidia kufanikisha vyema zoezi la sense ya watu ambayo inatarajiwa kufanyika hapo mwakani 2022.
ANGALIA TAARIFA YA HABARI HII KWAKUBOFYA HAPO CHINI.