Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu sifa za simu ya Infinix HOT 11.
Muonekano wa simu ya Infinix HOT 11.
…………………………………………..
Kampuni ya Infinix Hivi karibuni imezindua simu mpya ya Infinix Hot 11, na katika pitapita zangu nimebaini simu hii inafanya vizuri sana sokoni zaidi ya kuziacha brand za simu nyengine kwa asilimia kubwa.
Akizungumzia sifa simu ya Infinix HOT 11, Afisa Uhusiano wa Infinix, Bi. Aisha Karupa, amesema kwa upande wa sifa za ndani, Infinix Hot 11 inakuja na sifa bora kama vile, chipset ya MediaTek Helio G37, machaguo ya RAM ya GB 4, uhifadhi wa ndani wa kati ya GB 64 na GB 128, Infinix Hot 11 inakuja pia na kioo cha IPS LCD, chenye Inch 6.82 HD+. Mbali na hayo simu hii inakuja na kamera tatu za MP 50, MP 2, na QVGA. Bila kusahau battery kubwa ya 6000 mAh.
Bi. Karupa amesema kwa upande wa upande wa muundo, Infinix Hot 11 inakuja na rangi tatu ambazo ni Polar Black, Green Wave, Purple. Mbali ya hayo simu hii imetengezwa kwa Glass kwa mbele, plastic kwa, nyuma na frame ya plastic. Kwa upande wa kushoto kuna sehemu ya kuweka laini za simu pamoja na sehemu ya
Memory Card.
Amesema kuwa simu hii ya Infinix Hot 11 inakuja na uwezo wa kuchukua Memory Card yenye uwezo wa hadi GB 256, na hii ikiwa bila kuzuia wewe kuweka line zako bili kwani sehemu ya memory card inajitegemea.
Kwa upande wa display, Infinix Hot11 inakuja na display ya Inch 6.82 FHD, diplay hii inafanana kidogo kwa muonekano na toleo la mwaka jana la Infinix Hot 10 lakini pia kuna tofauti kubwa sana. Infinix Hot 11 inakuja na kioo chenye uwezo wa 90 Hz refresh rate, pamoja na resolution ya hadi 1080 x 2480 pixels.
Processor
Kwa upande wa processor, Simu hii ya Infinix Hot 11 inakuja na processor ya Helio G37 ambayo ni processor bora sana ambayo hii inaweza kusaidia simu kufanya kazi zote kwa ubora zaidi, ikiwa pamoja na kufanya simu kudumu na chaji zaidi. Kama wewe pia ni mpenzi wa game pamoja na kutumia internet basi utafirahia processor hii kwenye simu mpya ya Hot 11.
Battery.
Kwa upande wa battery, Infinix Hot 11 inakuja na battery kubwa ya 6000 mAh Battery, battery ambayo ina uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu kulingana na matumizi yako ya kila siku. Ukiwa unacheza game unaweza kucheza kwa muda wa zaidi ya masaa kumi na matatu na kubakiwa na battery angalu asilimia 30 kulingana na aina ya game unayo cheza.
Kamera.
Kwa upande wa kamera simu hii inakuja na kamera nzuri sana ambazo ni bora kulinganisha na simu nyingi. Infinix Hot 11 inakuja na kamera ya selfie ya MP 8 ambayo inasaidiwa na Dual-flash kupiga picha nzuri zaidi, mbali na hayo kwa nyuma simu hii inakuja na kamera kuu ya Megapixel 50 na nyingine mbili ambapo kwa ujumla unapata kamera tatu.
Kamera zote za mbele na nyuma zinakuja na uwezo wa kuchukua video hadi 1440p@30fps, hii ni moja kati ya sifa ambazo huwezi kuona kwenye simu nyingi za bei hii.
Pia kamera zote za mbele na nyuma zina portrait bokeh mode ambapo unaweza kuziba vitu vya nyuma na kuchukua picha ya mtu au kitu pekee kwa mbele.
Infinix Hot 11 pia inakuja na Night Mode kwenye kamera zote za mbele na nyuma, na pia unaweza kupiga picha zenye ubora sana kwa kutumia Night Mode.
Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii na basi Hot 11 itakuapa uwezo wa kuchukua picha bora sana za kuweka kwenye mitandao ya kijamii.
Amefafanua kuwa upatikanaji wa Infinix Hot 11 inakuja kwa bei nafuu na unaweza kupata sehemu yoyote Tanzania nzima ikiwa na ofa ya GB 78 za Tigo Mwaka Mzima lakini pia unaweza kununua Infinix Hot 11 kwenye maduka ya Infinix Tanzania nzima.