Monday, November 25

WACHEZAJI ZECO PEMBA ZIARANI MKOANI TANGA KUJIPIMA NGUVU NA TIMU MBILI

 

NA ABDI SULEIMAN.

MSAFARA wa wachezaji 28 na viongozi wanne wa timu ya Shirika la Umeme ZECO Tawi la Pemba, wamewasili salama mkoani Tanga kwa ziara ya siku tatu ya kimichezo.

Timu hiyo imewasili salama Disemba 24, ikitokea Kisiwani Pemba na Disemba 25 kuanza ziara yao ya kimichezo kwa kucheza na timu ya Black Worriors YA Tanda.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, afisa Uhusiano wa ZECO Pemba Amour Salum Massoud, alisema wachezaji, viongozi na mashabiki wao wamefika salama na kuwa na afya nzuri hasi sasa.

Alisema lengo la ziara hiyo ni kubadilishana uzoefu baina ya wachezaji wa ZECO na Tenesco Tanga, pamoja na kujiandaa na mashindano ya Mawizara yanayotarajiwa kuanza mwakani.

Amour alisema katika ziara hiyo wamepanga kucheza michezo miwili ya kirafiki, baina yao na Weyenji wao Tenesco Tanga na Black Worrios.

Aidha alisema katika mchezo wa kwanza ZECO Pemba ilifanikiwa kuibuka mshindi baada ya kuifunga Black Worrios bao 2-1 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Mzingani mkoani Tanga.

Aidha afisa huyo uhusiano, aliwashuruku wadau na wachezaji, viongozi wa ZECO kwa kufanikisha safari hiyo, ambayo itajenga uhusiano mwema kwenye kazi na michezo pia.

MWISHO